HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » VIJANA WANAODHANIWA KUHUSIKA NA SHAMBULIO LA KIGAIDI NCHINI UFARANSA WAKAMATWA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mtuhumiwa  Cherif Kouachi (kushoto) na ndugu yake Said Kouachi.
Ndugu wawili na kijana mmoja jana walielezewa kuwa ndiyo watuhumiwa watatu wanaohusishwa na shambulio la kigaidi jana dhidi ya jarida lenye kupinga Uislam nchini Ufaransa liitwalo Charlie Hebdo mjini Paris ambapo watu  12 waliuawa na saba kujeruhiwa.
 Polisi wakiendesha oparesheni ya kuwakamata watuhumiwa katika  kitongoji cha  Croix-Rouge eneo la Reims, kaskazini mwa Ufaransa.
Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na  mhariri mkuu, wachoraji wanne wa vikatuni na polisi wawili.  Inasemekana sababu ya kuvamiwa kwa ofisi za jarida hilo ni kuchapisha vikatuni vyenye kukashifu dini ya Kiislam.  Washambuliaji hao walitoroka baada ya shambulio hilo.

 Kikosi maalum cha kupiga vita ugaidi cha Ufaransa kikiwa kazini kuwasaka watuhumiwa.
Watuhumiwa hao ni  Said Kouachi (34), Cherif Kouachi (32) wote wakazi wa jiji la Paris, ambao ni pamoja na Hamyd Mourad (18) kutoka mji wa kaskazini-mashariki wa Reims, Ufarransa, aliyejisalimisha polisi baada ya kuona katika vyombo vya habari alikuwa anatafutwa. Hivi sasa polisi wanawatafuta ndugu hao wawili katika eneo la Croix Rouge hulo Reims.
 Polisi wakilinda jengo moja huko Reims wakati wapelelezi wakiendesha shughuli zao kuhusiana na shambulio hilo la kigaidi.
Askari wapelelezi wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo sehemu mbalimbali.


CHANZO: DAILY MAIL

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: