Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
KAMATI KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo
tarehe 28/8/2015, kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na moja alasiri,
kimeazimia yafuatayo;
> Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, msanii wa Chama na Kada wa muda
mrefu Mheshimiwa John Damian Komba.
Mwenyekiti wa CCM, Mhe Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea
kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa Chama hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye
uchaguzi na pengo ambalo ni vigumu kuliziba.
CCM imepata pigo na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti inatoa
pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kapteni John Damian Komba. Kazi yake kubwa ndani ya Chama itaandikwa katika historia
iliyotukuka ya Chama Cha Mapinduzi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
> Pia, kutokana na Kikao cha Kamati Kuu iliyopita
iliyoiagiza kamati ya maadili kuwaita na kuwahoji wanachama na viongozi watatu
waliotajwa kuhusika na kashfa ya Escrow.
@ Mheshimiwa Anna Kajumulo Tibaijuka
@ Mheshimiwa William Mganga Ngeleja
@ Mheshimiwa Andrew Chenge
Baada ya Kamati ya Maadili kuwahoji, Kamati Kuu imeazimia
kuwasimamisha kuhudhuria vikao ambavyo wao ni wajumbe ikiwemo Kamati kuu kwa
Mama Tibaijuka na Halmashauri Kuu ya Taifa kwa Mheshimiwa Chenge na
Ngeleja.,wakati ambapo kamati ndogo ya maadili ikiendelea na uchunguzi wa
kuhusika kwao katika kashfa hiyo.
> Pia, Kamati Kuu imejadili suala la Adhabu iliyotolewa
kwa wanachama sita ambao walibainika kuvunja Kanuni na sheria za Chama kwa
kuanza Kampeni kabla ya wakati na imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuendelea
kuchunguza mienendo ya wanachama hao katika kipindi walichokuwa wanatumikia
adhabu zao. Na kisha taarifa hiyo ya Kamati ndogo ya maadili itawasilishwa kwa
Kamati Kuu.
No comments:
Post a Comment