Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kanisa la lisilo rasmi la Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe,wilaya ya Kinondoni,jiji Dar limeamuriwa kuondoka mara moja na kuwacha eneo hilo wazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wa kawe. Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu lemekuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu na kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa wakazi wa maeneo hayo.
Barua ya kumfungisha viragao Mchungaji Josephat Gwajima
Katika Barua iliosainiwa na
Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa shirika la nyumba la Taifa imesisitiza
kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha shughuli
zake lakini shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo
kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo,kwani shirika hilo
limeshaanza kutumia Viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa KAWE
ikiwa ni ujenzi wa makazi n.k Bw Masika ametoa siku 30 tu ili
Mchungaji Gwajima kujitayarisha na kuwacha viwanja hivyo wazi kwa ajili
ya maendeleo ya wananchi.
No comments:
Post a Comment