Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Wafanyakazi wa ofisi za Manispaa ya Dodoma wakumpa kichapo kibaka aliyefahamika kwa jina la Lardsraus Haule alikamatwa akikwapua kofia [Willcape] za matairi ya Gari la mtangazaji wa TBC Victoria Patrick lililokuwa limeegeshwa nje ya ofisi hizo, huku askari Polisi akijaribu kuwazuia Bila mafanikio. (Picha na John Banda wa Pamoja Blog)
Mwanadada Victoria Patrick ambaye ni mtangazaji wa Televisheni ya Taifa [TBC] akionyesha kusikitika huku Mmoja wa wafanyakazi wa Manispaa ya Dodoma akiwa ameshika Moja ya kofia (Willcape) za Tairi za gari la mtangazaji huyo zilizokuwa zimechomolewa na kibaka aliyekutwa nazo.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kibaka Lardsraus Haule Mkazi wa Kizota manispaa ya Dodoma akidhitiwa na Askari wa kikosi cha FFU wakati alipokuwa akipelekwa Kituo cha polisi cha kati huku akiwa amebeba na kizibiti chake cha Kofia za Tairi alikutwa nazo akikwapua nje ya ofisi za manispaa hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe, Felista Bura akimuhoji kijana Lardsraus Haule mkazi wa Kizota alieyekutwa akikwapua kofia za tairi za Gari la Mfanyakazi wa TBC lililokuwa limeegeshwa nje ya ofisi za manispaa hiyo.
Ladsraus Haule aliyekamatwa akikwapua akiwa katika ofisi ya Meya wa manispaa ya Dodoma
No comments:
Post a Comment