HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » ALIYEKUWA MLINZI WA DK.SLAA AKANUSHA MADAI YA KUTAKA KUMUUA BALI ALILAZIMISHWA KUKIRI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Khalid Kangezi akitoa ufafanuzi mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
Aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Khalid Ahmada Kangezi amekanusha taarifa iliyotolewa na viongozi wa chama chicho kwamba alitaka kumuua bosi wake, Dk. Wilbroad Slaa.
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema siku ya kifo cha marehemu Kapteni John Komba alikuwa akitokea nyumbani kwake Mwenge akielekea kazini nyumbani kwa Dk. Slaa ambapo baada ya kufika getini aliambiwa na mlinzi wa geti hilo kuwa haruhusiwi kuingia ndani na alipouliza sababu alijibiwa kuwa taarifa imetoka kwa mke wa Dk. Slaa.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Alipoendelea kuhoji alipewa majibu  kwamba hapaswi kuendelea kumuuliza maswali ndipo aliamua kurudi tena nyumbani kujipanga kwa siku ambayo ingefuatia huku akiendelea kufanya juhudi za kumpata Dr. Slaa ili aweze kumuuliza sababu kuu ya kuzuiwa kuingia ndani.
Siku iliyofuatia ambayo ilikuwa Jumatatu ambapo Komba alikuwa anatakiwa kuagwa rasmi, alidamka asubuhi na mapema kuelekea nyumbani kwa Dk. Slaa kwani alijua kuwa naye angetakiwa kuungana na viongozi wengine kuuaga mwili wa marehemu.  Kwa bahati nzuri alifanikiwa kumkuta nyumbani japokuwa alizuiwa tena kuingia ndani ila majibu aliyopewa na Slaa ni kuwa aongee na mkewe wamalizane mgogoro wao na yeye akasema  hakutaka kuingilia mgogoro huo.
Kangezi aliongeza  kuwa hakutarajia kama mke wa Slaa angekuwa na mgogoro naye kwani walikuwa wakiitana mtu na kaka yake kwa vile wanatoka Mkoa wa Kagera.
Kangezi aliendelea kuelezea kuwa hakuamini kama kweli angeweza kufungiwa nje ya geti la nyumba kutokana na jinsi alivyokuwa akihangaika katika kuhakikisha ulinzi wa Dk. Slaa kwa nguvu ya hali ya juu kutokana na masuala ya vyama na ameishi naye kwa muda wa zaidi ya miaka 14 bila shida wala tuhuma yoyote.
Baada ya kukosa maelewano nyumbani kwa Dk. Slaa, aliamua kwenda katika ofisi za chama hicho zilizoko Kinondoni kwa ajili ya kuonana na kiongozi wake ambapo baada ya kufika alidai alizuiwa na viongozi wa chama hicho tena wakimtaka kuingia katika chumba maalumu kwa ajili ya kuchukua mahojiano naye ambapo  alifanya kama alivyotakiwa.
Aliwataja viongozi wa chama hicho aliowakuta humo ambao tayari walimwamuru kuvua nguo zake zote na kubakia kama alivyozaliwa huku akitishiwa kuuawa. Humo alitakiwa kueleza mahusianao yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Philip Mangula, na watu wa usalama wa taifa ambapo alisema alisulubiwa kwa muda wa saa sita na akitakiwa kuandika katika karatasi kukiri kuwa kweli anawasiliana nao na kutokana na kipigo alichokuwa akikipata,  akihofia kuuawa, aliamua kutii matakwa yao.
Siku hiyohiyo majira ya usiku alipelekwa katika hoteli iliyoko maeneo ya Sinza–Madukani ambapo alipakizwa katika gari lililokuwemo mwanasheria wa chama chicho, Mabere Malando, hadi kwenye hoteli waliyokuwa wamechukua vyumba na kumwingiza ndani ambako walianza tena kumsulubu hadi akaishiwa nguvu na akitakiwa tena aandike kuwa alikuwa na mpango wa kumdhuru Dk. Slaa kwa kumpa sumu,
Kutokana na uchovu aliokuwa nao aliamua kukiri kufanya hivyo huku akirekodiwa.
Alimalizia kwa kusema kuwa hajawahi kufanya jambo lolote la kutaka kumdhuru Slaa,  na hata kiasi cha fedha kilichotajwa kuingiziwa na watu wa usalama wa taifa si kweli na hawezi kutunza fedha katika simu.  Alieleza pia kwamba amefanya mambo mengi kwa Dk. Slaa na hivyo hawezi kumdhuru licha ya kufahamu siri zake nyingi. 

CHANZO: GPL

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: