Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akiongea na wananchi wa Misungwi baada ya kifo cha Magata Edson.
Mmoja wa wananchi wa Misungwi akimuuliza swali Mkuu wa Mkoa, Mhe. Mulongo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUSOMA HAPA CHINI
Ndugu wa Magata Edson wakilia kwa simanzi
Wananchi wa Wilaya ya Misungwi jijini Mwanza wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa.
Mhe. Mulongo akizidi kuongea na wakazi wa Misungwi.
MKUU wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amewaomba wananchi wa wilaya ya Misungwi kusubiri matokeo ya uchunguzi kuhusu madai yao kwamba jeshi la polisi wilayani humo linahusika na kusababisha kifo cha Magata Edson baada ya kumpa kipigo kikali.
Habari kutoka kwa wananchi mbalimbali wa Misungwi zinasema Edson alikuwa mfanyakazi wa gesti inayojulikana kwa jina la Recho Guest House ambapo usiku wa tarehe 14 mwezi huu, akiwa kwenye eneo lake la kazi, walikuja vijana wawili na msichana mmoja wakitaka kukodisha chumba cha kulala.
Inasemekana aliwahudumia na muda si mrefu mmoja wa wale vijana akatoka, wakabaki msichana na mvulana mmoja. Baada ya muda mfupi, msichana akatoka na kushitaki kwamba alikuwa amebakwa.
Baada ya Edson kupokea taarifa za binti huyo kuwa amebakwa ikabidi Machi 15 mwaka huu aende kituo cha polisi wilaya ya Misungwi kutoa taarifa za binti huyo kubakwa na mvulana waliyekuwa naye, kwani yeye ndiye aliyewahudumia chumba pale gesti.
Baada ya kufika kituoni hapo akakutana na yule binti aliyedai kubakwa na wote kwa pamoja wakawataja wahusika ambao walifuatwa. Baada ya watuhumiwa kupatikana, mmoja wao akasema hakumbaka msichana huyo bali walishindwana bei wakati tayari walikuwa wameshafanya tendo la ndoa.
Hapo polisi walianza kumwambia marehemu Edson aandike na akiri kuwa na yeye alihusika na ubakaji huo lakini alikataa.
Baada ya kukataa kuandika maelezo ya madai ubakaji, inasemekana polisi waliokuwa zamu siku hiyo wakamshushia kipigo kilichopelekea kutojitambua na kutupwa mahabusu.
Wakati akiwa mahabusu, mahabusu wenzake wakawaita polisi na kuwaambia kuwa hali ya Edson ilikuwa mbaya kutokana na kipigo alichokipata.
Hivyo alikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi ijulikanayo kama Mitindo na kupewa huduma ya kwanza. Kutokana na kuwa alikuwa amepigwa kupita kiasi, ikabidi apelekwe hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza ambako ndiko alifariki.
Awali, Machi 24, baada ya wananchi kupata taarifa za kifo cha Edson kufuatia kutibiwa kwa siku nne, waliamua kwenda kituo cha polisi Misungwi ili kutaka kujua kisa cha mwenzao kufariki na nini kingefuata baada ya hapo.
Wakati wakielekea kwenye kituo hicho ghafla walianza kupigwa mabomu ya machozi huku wakitawanywa wasifike kituoni hapo. Wananchi hao baada ya kuona hivyo ikabidi wakae kikao cha dharura ili kujua nini cha kufanya.
Baada ya kikao hicho wakaamua mambo mawili: kwanza, polisi waliopanga kwenye nyumba za wananchi hao warudishiwe kodi zao na kuondoka mara moja kwenye nyumba hizo, pili wakaiomba serikali kuhakikisha wafanyakazi maofisa wa upelelezi ndani ya wilaya hiyo wahamishwe na waliosababisha kifo cha marehemu wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Baada ya maoni hayo kupendekezwa yakapelekwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magessa Mulongo, ili aweze kutoa idhini ya maombi yao, lakini mambo yakawa tofauti.
Alipokwenda kuwapa pole alisema ofisi yake ilikuwa inafanya uchunguzi kubaini waliofanya kosa hilo na kwamba polisi waliotuhumiwa kuhusika walikuwa wanashikiliwa hadi uchunguzi utakapokamilika.
Mulongo alipoulizwa hatima ya polisi hao, aliwataka wananchi waache maneno yenye kujenga chachu ya uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao.
“Ni lazima tuwe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu kwetu na endapo uchunguzi kuhusu tukio hili utakamilika mapema, basi kila mtu atapata haki yake,” alisema.
Chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment