RAIS KIKWETE NA VIONGOZI MBALIMBALI WAHANI MSIBA WA KAPTENI KOMBA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Rais Jakaya Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole jana na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM marehemu Kapteni John Komba nyumbani kwake Mbezi kwa Komba jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo walipokwenda yeye na Rais Kikwete  kutoa pole na kuifariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015.
Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete
wakimfariji familia ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Rais Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma kikwete wakiwafariji wasanii wa Tanzania One Theatre kufuatia kifo cha kiongozi wao,  Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Marehemu Kepteni John Komba aliyefariki dunia jana nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Komba jijini Dar es salaam leo March 1, 2015
 Watoto wa marehemu, Andrew Komba (wa pili kulia) na George Komba kulia wakiwa na waombolezaji wengini nyumbani kwao Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Mbunge wa Monduli.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Komba (katikati) ni mke wa marehemu, Salome Komba. 
Lowasa akitita jambo na mtoto wa marehemu John Komba, Andrew Komba. 
 Mbunge wa Sengerema William Ngeleja akiwa na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa wakiwa katika msiba wa marehemu Kapteni John Komba. (Picha na Francis Dande)
Mbunge wa Sengerema William Ngeleja akiwa na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa wakiwa katika msiba wa marehemu Kapteni John Komba. 
 Rais Jakaya Kikwete akiwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walipokuwa kuhani msiba, nyumbani kwa Kapteni Komba, Mbezi Mbeach, Dar es Salaam
 Nape akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu John Komba
Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye akimfariji mjane wa aliyekuwa mbunge wa Mbinga, na Mjumbe wa NEC, CCM, John Komba. Picha zote na Adam Mzee.

Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhani msiba wa Kapteni John Komba ambapo alisema Komba alikuwa shuhuda kwenye mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na Malawi.

No comments

Powered by Blogger.