HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » SAA SITA ZATUMIKA NA POLISI KUMUHOJI DK. SLAA KUHUSIANA NA TUHUMA ZA KUTAKA KUWEKEWA SUMU NA MLINZI WAKE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa (kulia) akitoka Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam leo huku akiambatana na wanasheria wake, John Mallya (kushoto) na Nyaronyo Kicheere ambapo aliandika maelezo na kuhojiwa na Polisi kwa saa sita kuhusiana na tuhuma za kutaka kuuwawa na mlinzi wake, Khalid Kagenzi. (Picha na Francis Dande)
  Dk. Willibroad Slaa akiizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa maeleza na kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kituo Kikuu cha Kati.


ENDELEA KUSOMA  HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


 Dk. Willibroad Slaa akiizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa maeleza na kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kituo Kikuu cha Kati.
Mlinzi mpya wa Dk. Willibrod Slaa akimfungulia mlango.


Na Mwandishi Wetu

SIKU mbili baada ya kuwachiwa mtuhumiwa Khalid Kagenzi anayedaiwa kutaka kumuuwa kwa sumu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hatimaye Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Willibrod Slaa, naye amehojiwa leo.
Dk. Slaa alifika Kituo Kikuu cha Kati majira ya saa nne asubuhi kwa ajili yakuhojiwa na kuandika maelezo kuhusu tukio lakutaka kuuawa kwa kulishwa sumu.
Katika mahojiano hayo, Dk. Slaa aliongozana na wanasheria wake Nyoronyo Kicheere na John Malya, yalichukuwa muda wa saa sita huku baadhi ya wananchama waliombatana naye wakimsubiri nje.
Baadhi ya viongozi aliyoongozana nao walikuwa ni Profesa Abdallah Safari ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho Bara, Godbles Lema na John Heche.
Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza mahojiano hayo, Dk Slaa, alisema kuwa maelezo hayo yatumika katika ushahidi kuhusu tukio hilo.

Aidha Diwani Ubungo (Chadema), Jacob Boniface, alikuwa akihojiwa hata hivyo hadi waandishi wanaondoka katika eneo hilo alikuwa hajotoka kituoni hapo.
Kufikishwa katika kituo hicho kumetokana na sakata Chadema kutoa tarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kulikuwa na mpango wa mlinzi wake Kagenzi kutaka kumuua kwa sumu.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: