WAFANYABIASHARA MKOANI MWANZA WAGOMA KUFUNGUA MADUKA WAKISHINIKIZA SERIKALI KUMUACHIA HURU MWENYEKITI WAO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Baadhi ya maduka katika mitaa mbalimbali mkoani Mwanza yakiwa yamefungwa huku wananchi wakihangaika kutafuta huduma hiyo huku wafanya biashara wakiwa kwenye makundi madogo madogo
 
 Hali ilikuwa hivi katika mitaa mbalimbali jijini Mwanza

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwenye Mtaa wa Liberty jijini Mwanza, wamegoma kufanya biashara zao wakidai mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara hapa nchini aliyekamatwa Dodoma kwa kosa la kuwahamasisha wafanyabiashara wasilipe kodi, aachiwe kutokana na kuwa hana kosa lolote.

Wakizungumza na vyombo vya habari, wafanya biashara hao wanaofanya hao wamesema: “Sisi tumechoshwa na tabia ya serikali kumkamata mwenyekiti wetu kwa madai kuwa alituhamasisha kutolipa kodi, jambo ambalo si kweli hivyo na sisi tutaendelea na mgomo huu kuishinikiza serikali kumuachia mwenyekiti wetu.”

Aidha, wafanyabiashara hao wameongeza kuwa imekuwa ni kawaida yao kutofanya biashara siku ambayo mwenyekiti wao huwa anakwenda kusikiliza kesi yake lakini kwa sababu serikali, kupitia mahakama, imekataa kutoa mdhamana kwa mwenyekiti wao,hawafungui maduka mpaka hapo atakapoachiwa.

Mgomo huo wa wafanyabiashara ulianza tangu jana Alhamisi ambapo wafanyabiashara wote wa mtaa huo waligoma kufungua maduka yao wakitaka serikali imwachie mwenyekiti wao aliyekamatwa mjini Dodoma kwa madai kuwa amewachochea wafanya biashara hao wasilipe kodi.

Nao wananchi wa jijini hapa wameeleza kero wanazokutana nazo wakati maduka hayo yanapokuwa yamefungwaambapo wanakosa mahitaji yao na hivyo kuathiri vibaya maisha yao.

Katika hatua nyingine,mtaahuo ambao mahitaji muhimu ya binadamu hupatikana, wafanyabiashara mbalimbali kutoka Ukerewe, Igombe, Sengerema na hata mkoani Geita ambao huja kuchukua mahitaji hapo, wamesema mgomo huo umeathiri vibaya hali katika maeneo yao.
CREDIT:GPL

No comments

Powered by Blogger.