HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » WATU WAWILI WAMEFARIKI BAADA YA BASI LA FM SAFARI KUGONGANA NA FUSO ENEO LA MIKUMI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujerihiwa baada ya basi la FM safari likitokea Dar es Salaam kwenda mkoani Mbeya kugongana uso kwa uso na fuso iliyo sheheni nyanya katika eneo la hifadhi ya mikumi barabara ya Morogoro Iringa.
Wakizungumza  baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lingine na hivyo kugongana uso kwa uso ambapo wametupia lawama baadhi ya abiria kuwachochea madereva kuendesha kasi na ambapo wameshauri vyombo vya usalama barabarani kuwachukulia hatua madereva wazembe wanaosababisha vifo visivyo vya lazima.
Baadhi ya wasamalia wema wakiendelea kuokoa abiria waliokuwa kwenye basi ilo lililopata ajali maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Hii ndio hali halisi ya magari baada ya kupata ajali eneo la Mikumi
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amewataja walio fariki katika tukio hilo kuwa ni Seth Mapunda ambaye ni dereva wa fuso na mwanamke mmoja ambaye hajafahamika majina yake na jeshi la polisi linamshikilia dereva wa basi kwa kusababisha ajali

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: