HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » KIJANA AKUTWA AKIWA HAI BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI KWA SIKU TANO NCHINI NEPAL

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Kijana aliyeokolewa baada ya kufunikwa na kifusi kwa siku tano wakati wa tetemeko la ardhi mjini Kathmandu.
Kufuatia tetemeko kubwa la aridhi kuukumba Mji wa Kathmandu nchini Nepal siku tano zilizopita, waokoaji wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya kufunikwa na vifusi vya jengo alilokuwemo wakati wa tetemeko hilo.
 Licha ya kuwa chini ya maporomoko ya vifusi hivyo kwa siku tano, taarifa zinasema kuwa kijana alisaidiwa na mwanya uliokuwa ukipenyeza hewa iliyomwezesha kupumua japo kwa shida. Makundi ya watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua macho yake. Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi.

 Zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki kutokana na janga hilo.
Wengi wa wahanga hao wanasubiri misaada ya chakula na maji safi ya kunywa huku mashirika ya kutoa misaada yakisema huenda ikachukua siku nyingine tano kabla ya kuwafikia baadhi yao kutokana na kuharibiwa kabisa kwa miundo mbinu.
Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada wakikadiria michango inayohitajika kuwa zaidi ya dolla millioni 415 kuisaidia Nepal katika kipindi cha miezi 3 ijayo.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: