MBOWE AFANYA MKUTANO WA HADHARA MJINI BUKOBA, MWALIMU NA NASSARI MAKAMBAKO

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akihutubia mamia ya wakazi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa jana.
Mratibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Ziwa Victoroia, Renatus Bujiku, akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Bukoba mkoani Kagera.



 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar) Mhe. Salum Mwalimu na Mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe Joshua Nassari wakihutubia wananchi wa Makambako, mkoani Njombe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana  kwenye Uwanja wa Azimio, ikiwa ni sehemu ya operesheni ya mafunzo kwa viongozi kukiandaa chama kwenda kushinda dola na kuongoza serikali.
 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar) Mhe. Salum Mwalimu akihutubia wananchi
  Gari iliyowapeba Naibu KAtibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar) Mhe. Salum Mwalimu na Mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe Joshua Nassari ikiwasili katika mkutano wa hadhara Makambako, mkoani Njombe
Sehemu ya wananchi kwenye mkutano huo

No comments

Powered by Blogger.