WAANDAMANI WAPAMBANA NA POLISI MJINI BALTMORE BAADA YA KIFO CHA MMAREKANI MWEUSI FREDDIE GRAY

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Gloria Darden, mama mzazi wa kijana Freddie Gray aliyekufa akiwa mikononi mwa polisi akiwa mbele ya jeneza lenye mwili wa mtoto wake wakati wa maziko yake. 
 Vurugu kubwa ziliibuka jana katika mji wa Baltmore kati ya polisi na waandamanaji waliokasirishwa na kifo cha kijana Mmarekani mweusi, Freddie Gray aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi. 

 Polisi wakiwa wamejipanga tayari kupambana na waandamanaji katika mji wa Baltimore, baada ya maziko ya kijana Freddie Gray ambaye ni Mmarekani mweusi aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi.
 Katika vurugu hizo, ulitokea uharibifu mkubwa wa maduka, magari na jeshi la polisi nalo limetoa taarifa likisema baadhi ya maofisa wake wamejeruhiwa kufuatia vurugu hizo.
Gari la polisi likiteketea kwa moto kufuatia vurugu katika ya waandamanaji na polisi katika mji wa Baltmore, Maryland nchini Marekani hapo jana.
Askari polisi wakimsaidia mwenzao baada ya kujeruhiwa na waandamanaji
Hali ya hatari na kutotembea hovyo imetangazwa katika mji huo kufuatia vurugu hizo.
Kifo cha Freddie Gray ambaye ni kijana mweusi mmarekani mwenya asili ya kiafrika kimesababisha maswali mengi kuhusu matumizi ya nguvu za ziada ya polisi dhidi ya raia wa marekani wenye asili ya kiafrika.
Hata hiyo Msemaji wa polisi wa Baltimore Captain Eric Kowalczyk amesema vurugu hizo pia zimesababisha maafisa wake kujeruhiwa na wengine wapo katika hali mbaya.


No comments

Powered by Blogger.