Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Diwani wa Soko la Tazara Vetenary, Zahoro Maganga akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu alipotembelea maeneo yaliyoharibiwa na mvua akiongozana na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) jinsi maji yanavyotakiwa kufuata mfereji huo ambao haupitishi maji kupeleka katika mfereji huo .
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) katika ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam (kushoto) ni Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama.
Mhandisi Mradi Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Ngusa Julius (wa pili kulia) akimwelekeza jambo Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (aliye vaa kofia) wakati wa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya jimbo lake yaliyo haribiwa na mvua na kusaidia kutowa Mashine ya kuondoa maji hayo yaweze kuondolewa (kushoto) ni Katibu wa Kamati ya maafa na miundombinu ya Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke Morocco Milanzi na kulia ni Naibu Meya Manispa Temeke Juma Mkenga.
Katibu wa Kamati ya maafa na miundombinu ya Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke Morocco Milanzi (wapili kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (wa pili kushoto), wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam na mbunge huyo kusaidia mashine ya kuyaondosha maji hayo.
Baadhi ya maeneo waliyo kumbwa na maji katika Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke
Mwenyekiti wa Serikali ya Mta wa Kilimahewa Tandika Devis Coner Mfaume Mbonde (kulia) akielekeza jambo wakati wa ziara ya Mbunge na viongozi wa Tanroads wakiangalia maeneo yaliyoharibiwa na mvua nakuahidi kufanyia marekebisho maeneo hayo.
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
No comments:
Post a Comment