Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Na Takdir Ali –Maelezo Zanzibar.
Viongozi wa vyama vya siasa na Dini wametakiwa kuwashajiisha wafuasi
wao kushiriki katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kujikinga
na matatizo mbali mbali yanayoweza kujitokeza ikiwemo kokosa haki zao.
Amesema Daftari la kudumu la wapiga kura lipo kisheria si kwa matakwa ya
kisiasa hivyo viongozi hao wanapaswa kutumia nafasi zao kuwaelimisha
wafuasi wao kushiriki kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
linaloendelea kuboreshwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Ayub Mohd
Mahmoud wakati alipokuwa akifungua semina ya kutoa elimu ya
uandikishaji na uendelezaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa vijana
wa Wilaya ya Magharib A na B hapa Mwera Wilaya ya Magharibi B.
Amewaaleza vijana kuwa mara baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama
vingi vya siasa mwaka 1992,hali ya siasa Zanzibar haikuwa nzuri lakini
juhudi za viongozi walizochukuwa zimepelekea hali hiyo kutulia, kwa hiyo
si vizuri kwa wazee kuwaachia watoto wao au wajukuu zao Zanzibar
isiokuwa na amani na utulivu.
“Tumerithi nchi yetu kutoka kwa wazazi wetu ikiwa katika hali ya amani na
utulivu sivizuri hata kidogo kuwaachia watoto na wajukuu zetu wakiwa
katika nchi isiyokuwa na amani na utulivu,” alisema Ayub.
Aliongeza kuwa vijana kutoyajua yaliyopita na kujua yaliopo hivi sasa
yanapelekea kukosa nafasi ya kufikiri zaidi katika kutoa maamuzi jambo
ambalo amesema wanaweza kutoa maamuzi yasiyo sahihi.
Mapema akitoa maelezo Afisa uandiskishaji wa Daftari la kudumu la wapiga
kura Wilaya ya Magharibi Maalim Khamis Mussa amesema ili kufanikisha
Daftari hilo linaboreka zaidi mashirikiano ya pamoja ya wadau mbali
mbali ikiwemo vyama vya siasa, vyama vya hiari na Wananchi wenyewe.
Mwalimu Khamis amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa
wananchi kuwa kuna baadhi ya majina ya watu waliofariki ambao majina
yao hayajaondolewa katika Daftari la kudumu na kusema Tume ya
Uchaguzi haina uwezo wa kuwaondoa waliokosa sifa katika daftari hilo bila
ya wananchi kuenda kutoa vielelezo muhimu .
Wakichangia katika semina hiyo washiriki wameiomba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Tume ya Uchaguzi kuandaa mazingira
mazuri ya kuwawezesha wananchi kushiriki katika daftari la kudumu la
wapiga kura bila vikwazo vyovyote sambamba na kuweka wazi kuwa
watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ambao hawakupatata fursa hiyo
muhimu ya kushiriki.
No comments:
Post a Comment