Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungungumzwa katika mkutano wa siku mbili wa mashauriano kuhusu amani, umoja na utulivu wa nchi yetu ulioanza leo ambao utamalizika kesho. Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), ulifanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam leo asubuhi.
Brigedea Jenerali mstaafu, Francis Mbena akihutubia kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto ni Jaji mstaafu, Joseph Warioba, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo, Salim Ahmed Salim,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, Brigedea Jenerali mstaafu, Francis Mbene na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa.
Viongozi wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi wa vyama vya siasa wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Willibrod Slaa.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto),akiteta jambo na na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Salim Ahmed Salim (waliokaa mbele katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha mkutano huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad (kulia), akisalimia na mama Balozi Getrude Mongela katika mkutano huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Salim Ahmed Salim.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Salim Ahmed
Salim (katikati), akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, (kushoto) na Waziri
Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye wakati wakitoka kupiga picha ya pamoja
nje ya ukumbi huo.
(Imeandaliwa na mtandao wa http: www.habari za jamii.com)
(Imeandaliwa na mtandao wa http: www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment