
Aliyekuwa Sheikh mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shabani Simba enzi za uhai wake
Habari zilizotufikia hivi punde
zinaarifu kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba amefariki
dunialeo asubuhi.
Akidhibitisha kutokea kwa kifo hicho Shehe
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim amesema Mufti amefikwa
na umauti hii leo asubuhi.
"Ni kweli Mufti Mkuu wa
Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba amefariki hii leo asubuhi kwa maradhi
ya sukari na presha," alisema kwa ufupi Sheikh Alhhadi.
Kuhusu taratibu za mazishi amesema
taarifa kamili zitatolewa muda si mrefu.
Pamoja Blog inaungana na wailamu wote
nchini kufuatia na msiba huo mzito ambao umetokea.
INNA LILLAH WA INNA ILLAHI RAJIUN.



No comments:
Post a Comment