Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mamia ya Wakazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake
wakiwemo na Wageni mbalimbali kutoka nje ya Mkoa huu na nje ya Nchi
wamejitokeza kwa wingi kumzika marehemu Samuel Luangisa jana Jumatano
juni 3, 2015 nyumbani kwake Kitendaguro nje kidogo na Mji wa Bukoba. Marehemu Samuel Luangisa ni miongoni mwa waasisi wa Taifa
na katika vipindi tofauti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.
Mbunge wa Muleba Kusini Prof Anna Kajumulo Tibaijuka akiwa kwenye hali ya majonzi wakati wa mazishi ya marehemu Samuel Luangisa.
Taswira enzi ya uhai wa Marehemu Mhe. Samuel Luangisa
Merehemu Samwel Lwangisa alizaliwa mwaka 1932 na mauti yalimkuta New York Marekani tarehe 25.05.2015 na kuzikwa jana Jumatano juni 3, 2015 Nyumbani kwake Kitendaguro Bukoba.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akitoa neno kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye mazishi ya marehemu Samuel Luangisa yaliyofanyika mjini Bukoba

Kushoto ni Bw. Willy O. Ruta mkurugenzi wa kampuni mpya ya utalii Bukoba Tour akishuhudia Mazishi hayo.

Wengi
pia walifuatilia kupitia kwenye Tv Screen zilizokuwa ukumbini kutokana
na wingi wa Watu hivyo Tukio zima kuwafikia kupitia kwenye tv katika
sehemu walipokuwa maeneo hayo vyema.

Sehemu ya Baadhi ya Wanaumoja













Wageni Mbalimbali kutoka Nje ya Nchi walijumuika

Umati uliojitokeza katika mazishi.

Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana....Warumi 14:8






























No comments:
Post a Comment