Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi wa
Kata ya Buger wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha leo katika ziara ya siku
moja kuzungumza na wananchi baada ya mwananchi mmoja kuuawa kwenye msitu
wa Marang unaohifadhiwa na Shirika la Hifadhi ya Taifa(Tanapa).Waziri
Nyalandu ameunda Tume ya kuchunguza mgogoro huo ambayo itatoa
mapendekezo serikalini kwa utekelezaji.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na mmoja
wa wananchi wa Kata ya Buger wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha leo baada
ya kuhutubia wananchi hao na kuwahidi serikali kuwachukulia hatua askari
waliokiuka taratibu za maadili.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha,Cesilia Paresso akihutubia wananchi
wa Kata ya Buger na kuitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuzingatia
sheria na wananchi kulinda Msitu wa Marang kwaajili vizazi vijavyo.

Mkazi wa Kata ya Buger,Rehema Tango akitoa kero zake mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii.

sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huop ambao waliweza kutoa kero zao .



No comments:
Post a Comment