HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » BALOZI SEIF IDD APOKEA MSAADA WA KOMPYUTA KUTOKA KAMPUNI YA ZTE

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Ofisa wa Tawi la Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya Kisasa ya ZTE hapa Zanzibar yenye Makao Makuu yake Nchini  Jamhuri ya Watu wa China Bibi Coco Wang akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kumkabidhi msaada wa Kompyuta 10 kwa ajili ya wanafunzi wa Skuli zilizomo ndani ya Jimbo lake.

.................................................

Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya Kisasa ya ZTE yenye Makao Makuu yake Nchini  Jamhuri ya Watu wa China imeahidi kuendelea kuunga mkono harakati za kiuchumi za Zanzibar katika kuona wananchi wake wanafaidika na mfumo wa kisasa wa mtandao wa mawasiliano.

Ofisa wa Tawi la Kampuni hiyo ya ZTE liliopo hapa Zanzibar Bibi Coco Wang alisema hayo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi msaada wa  Kompyuta Kumi kwa ajili ya wanafunzi wa skuli zilizomo ndani ya Jimbo lake.

Akikabidhi msaada huo wa Kompyuta wenye thamani ya zaidi ya shilingi za Kitanzania Milioni 12,000,000/- Ofisini kwa Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar Bibi Coco Wang alisema Kampuni ya ZTE imejipanga kusaidia zaidi sekta ya elimu ambayo ndio msingi mkuu wa maisha ya mwanaadamu.


Bibi Coco alisema mfumo wa mafunzo katika vyuo na hata baadhi ya skuli za sekondari unaotumika katika Mataifa mbali mbali yaliyoendelea unaweza kutumika hapa Zanzibar endapo itaimarisha zaidi miundo mbinu ya mtandao wake wa  mawasiliano ya Compyuta.

Akipokea msaada huo wa Kampyuta Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliupongeza Uongozi wa Kampuni hiyo kwa moyo wake wa kujitolea katika kusaidia mtandao wa mawasiliano ya kisasa hapa Zanzibar.

Balozi Seif alisema Kampuni ya ZTE imeonyesha uungwana mkubwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kiasi ambacho unafaa kuigwa na Makampuni mengine makubwa katika kusaidia jamii.

Kampuni ya Kimataifa ya Mtandao wa Mawasiliano ya Kisasa ya ZTE yenye Makao Makuu yake Nchini  Jamuhuri ya Watu wa China ndiyo iliyofadhili mradi wa ufungaji Kamera za  kurikodi matukio mbali mbali ya kila siku (CCTV CAMERA) katika eneo la Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Ufadhili huo umekuja Zanzibar kufuatia ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyoifanya Nchini Jamuhuri ya Watu wa China mwishoni  mwa mwaka uliopita.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/7/2015.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: