HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MKUTANO WA WAKUU WA UTUMISHI WA UMMA WA JUMUIYA YA MADOLA WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


1 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa Jumuiya ya Madola Barani Afraik jana (Jumatatu Julai 13, 2015) Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku 3 unatarajia kufungwa Jumatano Julai 15, 2015. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani na Naibu Katibu Mkuu wa Jumiya hiyo, Bi. Josephine Ojiambo.
2
Naibu Katibu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akifuatilia kwa makini ufunguzi wa wa mkutano wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika jana (Jumatatu Julai 13, 2015) Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku 3 unatarajia kufungwa Jumatano Julai 15, 2015.
3
Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Serikali wakiwemo Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Watendaji wa Wizara, Taasisi na Wakala mbalimbali Serikalini wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika jana (Jumatatu Julai 13, 2015) Jijini Dar es Salaam.
4
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa Jumuiya ya Madola Barani Afraik jana (Jumatatu Julai 13, 2015) Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku 3 unatarajia kufungwa Jumatano Julai 15, 2015.
5
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Utumishi wa Umma wa Jumuiya ya Madola mara baada ya kufungua mkutano wao jana jumatatu Julai 13, 2015 Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku 3 unatarajia kufungwa Jumatano Julai 15, 2015.
6
Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Naibu Katibu Mkuu wa Jumiya ya Madola Bi. Josephine Ojiambo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika jana (Jumatatu Julai 13, 2015) Jijini Dar es Salaam.   Picha zote na Ismail Ngayonga


     Na Magreth Kinabo –Maelezo Dar Es Salaam 


RAIS Jakaya Kikwete amewataka Wakuu wa Utumishi wa wa Umma wa Jumuiya ya Madola kutoa maelezo ya kina kuhusu mipango ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuepusha malalamiko kwa umma .


Rais Kikwete aliitoa kauli hiyo jana (Jumatatu Julai 13, 2015) wakati akifungua mkutano wa 12 wa Wakuu wa Utumishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius K . Nyerere Jijini Dar es Salaam.


“Mara nyingi Rais anapouliza kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali anaambiwa inakwenda vizuri, wakati mambo hayaendi kama inavyotakiwa,” alisema Rais Kikwete.


Aliongeza kuwa changamoto wanazokabiliana wakuu hao wa jumuiya hiyo katika kutekeleza sera za Serikali ni uhaba wa fedha, hivyo utoaji wa maelezo sahihi unasaidia kupunguza changamoto mbalimbali.


Aliwataka wakuu hao kuwa na sera na mikakati yenye tija kwa wananchi ili kuboresha utoaji wa huduma bora.


Akizungumzia kuhusu mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa(BRN) alisema umesaidia kuleta uwazi na uwajibikaji na umeonekana kuleta manufaa katika kutekelezaji wa miradi hiyo ili kuwezea kufikia malengo.


Naye Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Josephine Ojiambo alisema kuna changamoto wanazokabiliana nazo ambazo ni utawala bora , haki sawa kwa wote, unyanyasaji wanawake, hivyo alimwomba kuendelea kutoa mchango wake kwenye masuala mbalimbali katika katika juhudi zake za kuwawezesha wanawake kupata nafasi mbalimbali kwenye ngazi za maamuzi na za kisiasa.


Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alisema ipo haja ya kubadilisha sera mbalimbali ili ziweze kukidhi matakwa ya wananchi kwa kubadilishana uzoefu wa kutoka nchi mbalimbali.

Mkutano huo umehudhuriwa na nchi 13 kati ya wanachama 18 wa jumuiya hiyo.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: