Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Jeshi la polisi mkoani Dodoma linamshikilia mtu mmoja mwenye asili ya kiasia baada ya kukutwa na mamilioni ya fedha kwenye begi akiwa kwenye Hoteli ya St.Gasper iliyoko mjini Dodoma.
Dereva wa gari lililokamatwa na fedha hizo Bw. Rashidi Shabani Nkungu mkazi wa Dodoma amesema alikodishwa na watu watatu wenye asili ya kiasia kutoka uwanja wa ndege kwenda Hoteli ya St. Gasper iliyoko mjini Dodoma.
Kwa upande wake meneja wa Hotel ya St. Gasper Bw,Denis Johanes amesema alibaini kuwepo kwa jambo lisilo la kawaida baada ya maelezo aliyompa wakati anatafuta chumba kutofautiana na aliyoandika kwenye kitabu cha wageni.
Alipotakiwa kueleza anakopeleka fedha hizo mtuhumiwa huyo pamoja na kukiri kuwa yeye ni mfanyakazi wa kampuniya Quality Group amesema alikuwa katika miamala yake ya kawaida.
Wakati jeshi la Poisi likiwa bado halijatoa ufafanuzi,kukamatwa kwa fedha hizo zinazokadiriwa kufikia zaidi ya milioni mia saba kumeongeza joto la wananchi na wana CCM wa mkoa wa Dodoma la kutoridhishwa na mwenendo wa matokeo ya vikao vinavyoendelea.
CHANZO: ITV TANZANIA




No comments:
Post a Comment