Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwenyekiti wa Chamacha Albino Tanzania (TAS), Bw. Ernest Kimaya (kushoto) akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walemavu wa Ngozi Tanzania kwenye viwanja vya Garden Mjini Iringa Mei 4, 2010.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania (Albino) ndugu Ernest Kimaya akimfariji Mama Maria Chambanenge wakati akipatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa kufuatia kukatwa mkono wake wa kushoto na watu walioshirikiana na mume wake na ambao walitiwa mbaroni na polisi mwaka 2013.
Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania (Albino) Ernest Kimaya akisisitiza jambo kwa wanahabari kufuatia kuvamiwa na kukatwa mkono kwa Mama Maria Chambanenge wa mkoani Rukwa Februari 19, 2013.
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Ernest Kimaya, akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Albinism Duniani katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Juni 13, 2015.
Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, wakiwa na Bw. Kimaya wakiwasikiliza watoto wenye albinism wakiimba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Albinism Dunia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Juni 13, 2015.
Mwenyekiti wa TAS, Ernest Kimaya, akimpokea Rais Kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro Juni 12, 2015. Rais Kikwete ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Albinism Duniani jijini Arusha 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Bw. Ernest Kimaya akisoma nakala za Katiba Inayopendekezwa yenye maandishi yaliyokuzwa mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro Machi 15, 2015.
Na Mwandishi Wetu, Korogwe
MWENYEKITI wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Ernest Njema Kimaya, kwa mara ya tatu amejitosa kuwania Ubinge katika Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akiahidi kushirikiana na wananchi kujiletea maendeleo.
Kimaya (48), ambaye amerejesha fomu jana Ijumaa, amesema anaamini kwa uzoefu wa uongozi alionao, anaweza kusaidia kutatua changamoto nyingi za wananchi wa Korogwe Vijijini, hususan suala la elimu, kilimo, afya na mindombinu ya barabara.
"Nina matumaini makubwa kwamba nikiteuliwa na chama changu kuwania nafasi hii adhimu, nitahakikisha tunatumia rasilimali nyingi zilizopo kujiletea maendeleo wenyewe," alisema Kimaya ambaye amekiongoza Chama cha Albino tangu mwaka 2000.
Kiongozi huyo, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupiga vita mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (albino), amesema kipambele chake kingine ni kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapatiwa fursa sawa katika shughuli zote za kijamii, ikiwemo elimu, afya, ajira na kadhalika.
Amesema jukumu lake la kwanza litakuwa kuwatambua watu wote wenye ulemavu jimboni humo, wakiwemo watoto ambao wameshindwa kupelekwa shule kwa sababu mbalimbali hasa za unyanyapaa, na kuhakikisha kwamba wanapatiwa fursa ya elimu kwani ni haki yao ya msingi ili waweze kujitegemea.
"Wapo walemavu wengi vijijini ambao kwa sababu mbalimbali wameshindwa kupata elimu ingawa wanao uwezo, nitashirikiana na serikali kuhakikisha wanapelekwa shule na kushirikishwa katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kupatiwa ajira," alisema.
Kuhusu uzoefu, Kimaya amesema kuteuliwa kwake na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014 kumempa uzoefu mkubwa wa kujenga na kutetea hoja zenye maslahi ya jamii.
Hii ni mara ya tatu kwa kada huyo wa CCM kuwania kuteuliwa kugombea Ubunge wa jimbo hilo, kwani aliwahi pia kugombea mwaka 2005 na 2010.
Kujitokeza kwa Kimaya kumepokelewa kwa mtazamo chanya na wananchi wengi wa Korogwe, ambao wamesema licha ya kada huyo kuwa na uwezo wa uongozi, lakini pia ni fursa mujarabu kwa watu wenye ulemavu kuchaguliwa ili waweze kujisemea na kuwasemea wengine.
"Uwakilishi wa walemavu katika vyombo vya kutunga sheria ni mdogo, ukiangalia maovu ambayo wanatendewa katika jamii, kuna kila sababu ya kuongeza uwakilishi, na hasa watu hawa wanapojitokeza kuwania nafasi za ushindani," alisema Jakson Shemndolwa, mkazi wa Mnyuzi wilayani Korogwe.
Shemndolwa alisema kwamba, uwezo wa uongozi hauangalii hali ya mtu ilivyo, bali namna anavyoweza kusimamia maendeleo na kutatua kero mbalimbali.
Hata hivyo, Kimaya atanakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Mbunge wa sasa, Steven Ngonyani 'Profesa Maji Marefu' pamoja na makada wengine sita ambao hadi kufikia jana walikuwa wamechukua fomu.
Wengine waliochukua fomu kuwania uteuzi ni pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini, Christopher Joseph Shekiondo, Edmund Mndolwa, Allan Samwel Michael Bendera, Abdallah Salum Nyanga, Fikiria Joseph Kolata na Steven Dastan Shetui.
Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni kesho Jumapili Julai 19 saa 10 jioni.
CURRICULLUM VITAE
1.
PERSONAL DETAILS
FIRST NAME : Ernest
SURNAME : Kimaya
OTHER NAME : Njama
DATE OF BIRTH : 1967
SEX : Male
MARITAL STATUS : Marriage
NATIONALITY : Tanzania
LANGUAGE SPOKEN : Swahili/English
PERMANENT ADDRESS : Box 9644 Dar
PHONE NO. : 0713
263196
E- MAIL ADDRESS : ernestkimaya@yahoo.com
2.
EDUCATION BACKGROUND:
Ø COURSE
IN COMMUNITY MAPPING AND THEATRE AGAINST AIDS: 2002 – BY UNAIDS
Ø COURSE
IN LIFE SKILLS : 2000 – BY UNCEF
Ø COURSE
IN ADMINISTRATION AND FINANCE MANAGEMENT: 1999 – BY ESAMI
Ø O.
LEVEL: 1985 – 1988 – SAME SECONDARY.
Ø PRIMARY
SCHOOL: 1978 – 1984 – SAME PRIMARY
SCHOOL.
3.
ATTAINMENT AND EXPERIENCE:
Ø Chairman
- Tanzania Albino Secretary from 2000 – to Date.
Ø Regional
Manager - Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) in Tanga
Region. 2007 – 2010.
Ø Vice
Chairman - Tanzania Albino Society: 1995
– 1999
Ø Secretary
- Albino Society, Tanga Region: 1991 –
1995
4.
AWARDS
Martin Luther King Award 2009 – From American Embassy.
5.
DATE OF PUBLICATION
6.
REFEREES:
1st REFEREE
NAME : Isack Kivuma Mlangwa
SEX : MALE
PLACE OF WORK : CLEARING
& FORWADING
COUNTRY : TANZANIA
ADDRESS : BOX 5930 TANGA
Phone No. :
E-mail Address :
2nd REFEREE:
NAME : Monica Kimaya
SEX : Female
PLACE OF WORK : Police
Force
COUNTRY : Tanzania
ADDRESS : Box 9644 Dar
es Salaam
PHONE No. : 225 02 754 594589
E-mail Address :
7.
ADDITIONAL:
Hobies: Reading Books, magazines, watching
comedies and helping people who are in need.
No comments:
Post a Comment