Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha Waombaji wa mikopo na Umma kwa ujumla kuwa muda wa kuwasilisha maombi ya mikopo umeongezwa mbele hadi tarehe 31 Julai, 2015.
Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika muda uliopangwa. Itakumbukwa kuwa, awali Bodi ilianza kupokea maombi kwa njia ya mtandao tarehe 4 Mei, 2015 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 30 Juni, 2015.
Kupitia taarifa hii, waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao hawajakamilisha maombi yao wanatakiwa kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa.
Bodi inapenda kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 31 Julai, 2015.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
No comments:
Post a Comment