HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » VIONGOZI WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO WAALIKWA UJERUMANI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo mama Anna Mghwira (kulia) akiongozana na katibu mkuu  Ndugu samson mwigamba na katibu wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ndugu Venance Msebo leo tarehe 15 julai 2015 wameanza ziara ya siku saba nchini ujerumani kwa mwaliko wa chama rafiki cha kijamaa (Die Linke Party).

Katika ziara hiyo pamoja na kutembelea die linke party, watapata fursa ya kutembelea ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani na pia watafanya mkutano na watanzania wanaoishi nchini ujerumani.
 katika mikutano hiyo na watanzania waishio nchini Ujerumani lengo kuu litakuwa kuwahamasisha kuchangia maendeleo ya nchi yao na pia kutafuta fursa kurudi nyumbani kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na kupiga kura ifikapo Oktoba mwaka huu.

Imetolewa na Afisa Habari,
ACT Wazalendo
Abdallah Khamis
15 julai 2015

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: