HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAMBO 7 AMBAYO VIONGOZI WANAWEZA KUSAIDIA WATU KUBADILIKA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Je ulishawahi kumbadilisha mtu tabia yake ofisini? Huwa inachosha sana na mara nyingi juhudi hiyo vile vile inaleta matokeo tofauti na ulivyotegemea.

Watu hukasirika wanapojaribu kurekebishwa, wanapunguza kufanya kazi n.k lakini kuna namna nzuri tu ambayo unaweza kufanya kazi na wenzako na kwa uzuri kabisa.
Kutokana na utafiti wa watu ambao wapo kwenye mazingira ya kazi, wanasema waliweza kuwafanyia utafiti mameneja kwenye tabia 49 na katika uwezo wao wa kuleta mabadiliko hasa katika ushawishi wa kuwezesha kupeleka taasisi inakotakiwa kwenda.
Walipoweza kuwaangalia wakakutana na tabia ambazo wengine zinawashusha hivyo kushindwa kuleta mabadiliko na wengine zimewapandisha na mabadiliko yameonekana kwenye taasisi zao.

Na vile vile waliweza kukutata na tabia ambazo hazisaidii kuleta mabadiliko kwa wengine na nyingine mbili hazina mabadiliko kabisa au huleta kidogo sana, na hapa ni mwongozo wakuweza kukusaidia kitu cha kufanya kama kiongozi;
  • Kuwa mpole na mwenye kujali watu. Samahani watu wa aina hii huwa wanakuwa wa mwisho kwenye kuleta mabadiliko Inawezekana ukaona ni rahisi kwamba ili ulete mabadiliko inakubidi uwe mpole na mwenye kutegemea mahusiano mazuri na watu wengine. Lakini hiyo si sababu.
  • Kuwapa wengine maelekezo, ushauri na mawazo kandamizi. Wanaopokea mawazo hayo huumizwa na kuudhika sana badala ya kuleta mabadiliko na mbinu hii mwengi hupenda kuanza nayo.
  • Wakati wakifanya uchunguzi huo wakagundua tabia ambazo zinakwenda moja kwa moja katika kusaidia kuleta mabadiliko, wakapata tabia saba. Hebu tuzitizame kama zina ukweli ndani yake kutokana na uchunguzi wao. Kuwapa motisha wengine. Kuna kanuni mbili zinazotumika unapojaribu kuwashawishi watu kuleta mabadiliko. Kwa upana wake ni “kuwasukuma” na “kuwavuta” hivyo basi viongozi wengine huwasukuma watu, kuwatumia vimemo vingi vya kukumbusha na hata kuchukua hatua ya kuwaonya wasipofanya. Huu ni mfumo ambao ni sawa na kuweka mikono nyuma na huku ukitegemea mabadiliko.
    Njia mbadala ni kuwavuta watu, hii inahusisha mtu mwenye kuonyesha ushawishi wa malengo na namna ya kuyafikia. Na njia hii inatumika vizuri pale ambapo ukianza kutafuta wengine wanafanya ili kukamilisha jambo gani na unahusiana nao ili uweze kuoanisha wanachokifanya ma malengo yanayotakiwa kufikiwa. Viongozi hawa hutoa maneno yenye hekima na kukuonyesha uhalisia wa mambo badala ya kukutisha. Na kitu kingine ni kupata muda wa kuongea na hao watu na kuelezea kwanini inatakiwa kufanyika hivyo unavyotaka ili yatokee mabadiliko.
  1. Kugundua matatizo . Watawala wengi ushauri wao ni kutaka watu wawe na uwezo wa kutatua matatizo, ila kuna hatua zinazokuja mapema. Kwanza ni kuweza kujua tatizo
au matatizo na uwezo wa kuyatafutia ufumbuzi hapo ni rahisi kupata mabadiliko.
3. Kuwa na malengo yanayoeleweka. Mabadiiko yanafanya kazi vizuri pale ambapo kila mmoja anatakiwa kufikia malengo hayo na kitu kingine katika malengo hayo kunatakiwa kuwa na mkakati unaowezesha kufikia malengo hayo.
  1. Kiongozi wenye mabadiliko huleta changamoto. Mafanikio mazuri ya kuleta mabadiliko yanahitaji kiongozi ambaye atatizama mbinu za kawaida na kuzipa changamoto hizo mbinu. Kwa lugha nyingine hubadilisha mbinu zile zilizopo na kuleta mbinu zenye tija zaidi.
  2. Hujenga kuaminika kwenye fikra zako . Hii yote inatokana namna ambavyo unaweza kukuza upeo wako wa kufikiri na namna unavyotafsiri mambo. Kiongozi mzuri anafanya maamuzi kwa umakini sana baada ya kufanya utafiti na kupata mawazo sehemu mbalimbali. Wanajua kutafuta ushauri sehemu nyingine na ushahidi kwamba wana ujasiri na nguvu wala si kwamba ni wadhaifu. Kutokana na uwezo wao wa kujenga imani katika maamuzi wanayofanya wana uwezo wa kubadilisha mwenendo wa maendeleo kwenye taasisi husika. Kama watu hawaamini maamuzi yako itakuwa ni vigumu kuwapata na kufanya mabadiliko unayoyahitaji.

  1. Ni watu jasiri . Mtu mmoja alisema hivi , “Huwezi kufanya jambo lolote kama huna ujasiri. Hiki ni kiwango cha hali ya juu cha ufahamu karibu kabisa na heshima.” Ukweli ni kwamba kila mwamko unaanzia kwa kiongozi, kwa kila mfanyakazi unayemwajiri, kwa kila mabadiliko ya utekelezaji unayoanzisha, kila bidhaa ambayo mnaitoa, na kila mazungumzo unayoyazungumza na kutoa rejea kwa wafanyakazi wengine na kwa kila uwekezaji katika vyombo vinavyohitajika marekebisho ili kuongeza ubora. Hivyo ujasiri unahitajika katika kila eneo.
Kuna wakati watu wengi husema “Mtizamo wetu ni vile ambavyo kiongozi wetu anafanya na hasa katika kufanya mabadiliko, inasababisha watu wawe tayari kuondoka kwenye mazingira ya kawaida waliyoyazoea na kufanya zaidi”
  1. Huyafanya mabadiliko kuwa jambo la msingi . Mabadiliko mengi huwa yanashindikana kwa sababu yanakuwa ni mija ya agenda nyingine nyingi. Lakini kiongozi aliye makini anataka mabadiliko ndio liwe jambo la kwanza na la msingi ili kuweza kusonga mbele. Unapokuwa wewe ni sehemu ya mabadiliko , utabadilisha kila sehemu ya maisha yako, sehemu zote nyumbani na kwenye biashara. Itasaidia kubadilika wewe mwenyewe.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: