Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Usishangae kuona makala hii kuhusu harusi. Naandika kutokana na uzoefu wa kuwa kwenye kamati nyingi za maandalizi ya harusi. Unapokuwa kwenye kamati hizo kuna vitu vingi ambavyo vimekuwa vikijitokeza na vijana wengi hatuvijui au kutotilia maanani na mwisho wa siku sherehe inakwisha na mambo ni kama ya sherehe nyingine ya ndugu yako au rafiki yako.
Kwa ufupi kunakuwa hakuna ubora wa harusi au mwenendo mzima unakuwa hauko vizuri.
Kuna familia ambazo wanajitahidi kupanga vizuri na kufanya sherehe vizuri na kuna nyingine zinaboronga na kuacha watu wakijiuliza tatizo lilikuwa nini?
Vitu vya kuzingatia kutokana na mtizamo wangu ni kama ifuatavyo:
Maharusi mnatakiwa kuandaa mpango wa sherehe mapema kabla ya ndugu na watu wengine kuwaandalia
Kuna watu wanashtuka kuhusu hili ila ninachotaka ujue ni kwamba sherehe ni ya kwenu ninyi maharusi mambo yanapokwenda vizuri hiyo ni kumbukumbu ambayo mtabakinayo maisha yenu yote na ikienda vibaya kumbukumbu hiyo ni ya kwenu ninyi hao ndugu na jamaa watakuwa nyumbani kwao na ninyi kwenu. Hivyo basi ninyi ndio mpango wenyewe na hivyo mnatakiwa kuiandaa sherehe yenu na namna mnavyotaka ionekane kabla ya mtu mwingine yeyote ili kumbukumbu yenu isiharibiwe na mambo kufanyika kama kawaida.



No comments:
Post a Comment