HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AZINDUA KAMATI ZA USHINDI ZA WANAWAKE KISIWANI PEMBA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.




Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wajumbe wa Kamati za Ushindi za Wanawake wa CUF kutoka Wilaya nne za Pemba huko skuli ya Fidel Castro.


Wajumbe wa Kamatui za Ushindi za Wanawake kisiwani Pemba wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mhe. Maalim Seif Sharif Hanmad mara baada ya kuzindua kamati hizo huko skuli ya Fidel Castro mkoa wa Kuisni Pemba.



Na. OMKR Zanzibar



Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad leo amezindua Kamati za Ushindi za Wanawake Kisiwani Pemba na kuwahimiza wajumbe wake kufanya kazi kwa bidii kukihakikishia ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.


Akihutubia katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano skuli ya Fidel Castro, mkoa wa Kusini Pemba, Maalim Seif amesema wanawake wana uwezo mkubwa wa kuwafikia wapiga kura popote pale walipo.


Amesema mchango wa wanawake katika uchaguzi ni wa kipekee na wamekuwa kama askari wanaoweza kutumwa sehemu yoyote ile na kwenda kufanya kazi kwa mafanikio makubwa.


Amewataka wanawake wa CUF katika kufanya kazi hiyo wawe na hekima na busara na wawafikie wanachama wa vyama vyote wawaeleze mipango na mikakati mizuri ya CUF katika kuwaletea maendeleo wananchi pale kitakapo kamata Serikali.


Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake CUF, Mhe. Zahra Ali Hamad amesema wajumbe hao wa Kamati za Ushindi wako tayari kutumia ushawishi walio nao kwa kupita nyumba hadi nyumba kuwahamasisha wanawake wenzao na vijana kukipa kura nyingi chama hicho.


Mapema katika risala ya Kamati hizo iliyosomwa na Bimkunga Hamad wamesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanawapatia kura na ushindi wa kihistoria wagombea Urais, Edward Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad kupitia ushirikiano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). 


Khamis Haji, OMKR

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: