Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili –MNH- imetoa mafunzo kwa watumishi wake kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu ambao umesambaa
na kusababisha watu 989 kuambukizwa ugonjwa huo jijini
Dar es salaam.
Mafunzo hayo ya siku saba ambayo
yanahusisha Wakurugenzi, Wakuu wa Idara , Madaktari, Wauguzi , Wafamasia pamoja
na Wahudumu yana lengo la kuwaelimisha
juu ya ugonjwa huo , jinsi ya kuzuia , kumtibu mgonjwa na kumtambua mtu mwenye
dalili za Kipindupindu.
Akielezea mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya magonjwa ya
dharura na ajali ambaye pia ni
Daktari Bingwa wa magonjwa hayo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dokta
JUMA MFINANGA amesisitiza kuwa chanzo kikuu cha
ugonjwa wa Kipindupindu ni uchafu lakini pia maji machafu yanachangia kwa asilimia kubwa kuenea
kwa ugonjwa huo.
Hivyo amewakumbusha wananchi
kuzingatia usafi kwa kunawa mikono kwa
sabuni na maji yanayotiririka , kula vyakula
vya moto , kunywa maji yaliyo safi na salama kusafisha mazingira na kwa wale wanaosafiri wametakiwa kutokula hovyo barabarani kwani hali bado ni tete.
Kwa mujibu wa Dokta MFINANGA Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea wagonjwa 20 ambao wanadalili za ugonjwa huo na kisha kupelekwa katika kambi za Kipindupindu.
Manispaa ya Kinondoni
inaongoza kwakuwa na wagonjwa 663, Ilala ina wagonjwa 246 na Temeke ina
wagonjwa 80.
Mafunzo hayo
yameanza leo yatamalizika Septemba 17 mwaka huu ambapo leo waaguzi 126 tayari wamepatiwa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment