Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Viongozi wa
taasisi za vijana kutoka kwenye nchini sita wamekutana mjini Bagamoyo kujadili
na kuandaa mtaala utakaotumika kuwafundisha vijana namna ya kufanya
ujasiliamali usioathiri mazingira “Green Entrepreneurship”.
Mkutano huo
ambao ulitanguliwa na ziara ya mafunzo kwenye Shirika la Maendeleo ya
Nishati Mbadala (TaTEDO), umewashirikisha viongozi wa taasisi za vijana
kutoka Slovenia, Italia, Nepal, Ureno, Argentina na wenyeji Tanzania walipata
fursa ya kujifunza namna ya uzalishaji wa nishati mbadala isiyoathiri mazingira.
Picha ya pamoja wakati viongozi hao walipotembelea TaTEDO.
Chris Ndallo
(kushoto), Mtendaji Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Vijana TYCEN akijadiliana
jambo na baadhi ya watumishi wa TaTEDO.
Viongozi wa taasisi za vijana, wakitazama baadhi ya miradi inayoendeshwa na TaTEDO wakati walipotembelea ofisi za shirika hilo.
No comments:
Post a Comment