Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kulia), akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa taarifa ya vituo vya afya nchini uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa wizara hiyo, Hermes Rulagirwa na Ofisa wa Tehama, Kenani Mwansasu.
Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa wizara hiyo, Hermes Rulagirwa (kulia), akizungumza na wanahabari.
Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Jengo la Ubungo Plaza.
Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Jengo la Ubungo Plaza.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imezindua mfumo mpya wa kuhifadhi taarifa za vituo vya huduma ya afya vya Serikali na binafsi katika ngazi ya kanda, mtaaa kijiji na mkoa nchini.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizindua mfumo huo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando alisema kupitia mfumo huo watumiaji watapata taarifa za vituo sahihi na namna vinavyotoa huduma.
Alisema mfumo huo utatumik kama chanzo pekee cha taarifa za vituo na mwisho utumiwe na wananchi kupata taarifa za huduma zinazotolewa na kituo husika.
"Mpango huu wa kielektroniki wa kuandaa mipango na kufanya maamuzi madhubuti wa sekta ya afya nchini, tunaomba na tunahitaji sana kushirikiana katika kuboresha huduma za afya na kuwatendea haki Watanzania," alisema.
Aliongeza kuwa utatengeneza namba maalum kwa kila kituo kitakachoingizwa na namba hiyo haitarudiwa hata kama kituo hicho kitafungwa.
Dk.Mmbando aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali kwa kuhakikisha wanaleta maendeleo nchini na kuwaaagiza waganga kuhakikisha wanafanya update kila wakati ili kuendana na wakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Tehama Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Hermes Rulagirwa alisema kupitia mfumo huo utatawawezesha kujua sehemu ya kituo kilipo na huduma wanazozitoa.
Alisema kabla ya kuzinduliwa kwa mfumo huo wapo waganga kutoka vituo mbalimbali nchini walipatiwa mafunzo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment