Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Wakimbizi kutoka nchini Burundi walioko katika kambi ya Nyarugusu wakiwa wamebeba shehena ya unga wa mahindi jana, muda mfupi baada ya kugawiwa chakula hicho Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililoweka kituo chake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Kinamama wakimbizi toka Burundi wakipata mgao wao wa unga unaotolewa kwa wakimbizi wanaohifadhiwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Serikali kwa kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa imeendelea kuhakikisha kuwa wakimbizi hawa toka Burundi wanapata chakula cha kutosha kwa ajili ya mahitaji yao.
Mkimbizi Irene Ntibelenda (katikati) akiwa pamoja na ndugu yake Sengiyu Mvajeme (kulia) baada ya kupokea mgao wa chakula unaotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililo na Kituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Kushoto ni mtoto wake aitwaye Nsengiyumva Idiphonce.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Josef Ntukugurya akifunga shehena ya unga wa mahindi jana, muda mfupi baada ya kupokea unga huo kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa, linashughulikia chakula (WFP), lililoweka kituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma
Sehemu ya
shehena ya chakula ukiwepo unga wa mahindi na mafuta ya kupikia ikiwa katika
ghala la kuhifadhia chakula lililopo katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu
iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Chakula hiki hutolewa na Jumuiya ya Kimataifa kama kupitia Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP) ili kusaidia wakimbizi
wanaohifadhiwa hapa nchini. (PICHA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
No comments:
Post a Comment