Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mgombea Urais wa Tanzania
kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa
UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwaaga wananchi wa Jiji la Mwanza, mara baada ya
kuhutubia Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Furahisha, Jijini
Mwanza Oktoba 12, 2015.
Watu wa huduma ya kwanza wa kikosi cha Msalaba Mwekundu, wakiwasaidia wananchi mbali mbali waliopoteza fahamu kutokana na kukosa hewa, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Furahisha, Jijini Mwanza Oktoba 12, 2015.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Juma Duni Haji, akiwahutubia wananchi, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Furahisha, Jijini Mwanza Oktoba 12, 2015.
Mwanasiasa Mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, akihutubia wananchi, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Furahisha, Jijini MwanzaOktoba 12, 2015.
No comments:
Post a Comment