Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
NYUMBA ya Naibu sheha wa shehia ya Tibirinzi
wilaya ya Chake chake Pemba, Bikombo Simai Juma (42), ambayo imedaiwa kuchomwa
moto na watu wasiofahamika kwa madai ya hitilafu za kisiasa, tukio hilo
lilitokea oktoba 26, majira ya saa 7:00 usiku, ambapo wakati huo alikuwa ndani
amelala na jumla ya watu 13 akiwemo mtoto mchanga wa mwezi mmoja, walisalimika
kufa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
: NYUMBA nyengine ilioko kando mwa nyumba ya
naibu sheha, eneo hilo la Tibirinzi, kijiji cha Minazini, ikiwa imechomwa moto
nyuma kwenye eneo la choo cha makuti, inayomilikiwa na Khamis Kassim Juma siku
hiyo hiyo ya Oktoba 26 usiku wa saa 7:00 ambapo matukio yote hayo hakuna
aliejeruhiwa.
NAIBU sheha wa shehia ya Tibirinzi wilaya
ya Chake chake Pemba Bikombo Simai Juma (24) akizungumza na mwandishi wa habari
hizi hayupo pichani, muda mfupi baada ya nyumba yake kudai kutiliwa moto na
watu wasiofahamika.
No comments:
Post a Comment