Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_71k-NpB7hod_tazRnedvWPVoaWW86w_6P9oGNXhPOIt7N9bDz6sSmk8AVipsis5b35ZMDwe__P06GDrONrep0rQTRnPob7sj7EpMzkRRQ9nKKMNyiM0UiNplp5mNaNMYXE1XsW_PvE_V/s640/Ministry%2527s+Header.JPG) |
Taarifa
zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi
Arabia
Mahujaji wengine wanane kutoka
Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji
ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa
kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia.
Kutambuliwa kwa mahujaji
hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania walipoteza maisha katika ajali hiyo
kufikia ishirini (20). Majina kamili ya mahujaji hao na vikundi
vilivyowasafirisha kwenda Makkah katika mabano ni Hamida Llyas Ibrahim (Khidmat
Islamiya), Farida Khamis Mahinda (Ahlu Daawa), Archelaus Anatory Rutayulungwa
(Khidmat Islamiya) na Said Abdulhabib Ferej (Ahlu Daawa).
Wengine ni Awadh Saleh Magram
(Khidmat Islamiya), Salama Rajab Mwamba (Khidmat Islamiya), Nuru Omar Karama
(Ahlu Daawa) na Saida Awaadh Ali (Ahlu Daawa).
Serikali ya Saudi Arabia
inaendelea kutoa taarifa zaidi za mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa
katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri
itakapokuwa inazipokea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
13 Oktoba, 2015
|
No comments:
Post a Comment