Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC ,CCM Makao Makuu Dodoma
akiwa ameshikilia kitabu cha Kanuni za Kamati ya Wabunge Wote wa Chama Cha
Mapinduzi.

Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo majina matatu yalipitishwa.
Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika
leo Novemba 15, 2015 mjini Dodoma imewateua wana-CCM watatu watakaopigiwa kura
na wabunge wote wa CCM ili kumpata mgombea wa CCM katika nafasi ya Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Walioteuliwa kugombea nafasi hiyo na Kamati
Kuu iliyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete ni pamoja na Naibu Spika aliyemaliza muda wake Ndugu JOB NDUGAI, Dkt.
TULIA ACKSON na Ndugu ABDULAH MWINYI.
Kwa upande wa Naibu Spika wa Bunge, mchakato
wa kuchukua fomu kwa wabunge wa CCM wanaoomba ridhaa kugombea nafasi hiyo
utaanza kesho Novemba 16, 2015 na kukamilika Novemba 17, 2015 saa kumi kamili
jioni.
Wana-CCM hao watatu watapigiwa kura na Kikao
cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM kitakachofanyika kesho Novemba 16, 2015 saa
nne asubuhi katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma ilikuchagua jina moja
kugombea nafasi hiyo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kuhusu nafasi ya Naibu Spika, alisema kulikuwa na kasoro za
kutofuata kanuni za chama ambapo hadi jana ni mwanachama mmoja tu ndiye
aliyekuwa amechukua fomu ya kugombea ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan
‘Zungu,’ lakini atatakiwa kuchukua fomu upya.
“Ibara ya 57,
Kanuni za kamati ya wabunge wote wa CCM toleo la 2010 toleo la nne 2011, mbunge
yeyote anayetaka kugombea nafasi ya Naibu Spika atatakiwa kuchukua fomu kupitia
kamati hiyo na atairudisha kisha kamati itakaa kupata jina moja,” alisema Nape.
Kwa mujibu wa maelezo hayo mbunge wa chama hicho anayetaka kugombea
Unaibu Spika, atatakiwa kuchukua fomu leo Novemba 16, kwa ada ya Sh 100,000
kisha atairudisha kesho Novemba 17, ndipo kamati itakaa kuchambua na kupitisha
jina moja.



No comments:
Post a Comment