HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » UPDATES: RAIS MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU WA TRA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Raisi wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.

Hatua hiyo imekuja baada kubaini kupitishwa kwa makontena zaidi ya 300 na kusababishia hasara Serikali ya zaidi ya shilingi bilioni 80.

Rais Magufuli pia amemteua  Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo mpaka hapo uchuguzi utakapo kamilika.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Katibu Mkuu Kingozi, Balozi Ombeni Sefue Ikulu jijini Dar es salaam, imewataka maofisa wote wa TRA kutosafiri nje ya nchi mpaka pale uchunguzi dhidi yao utakapo kamilika.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: