Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Leo eneo La Chanika, Dar es salaam mida ya saa 9 jioni majambazi wapatao zaidi ya 8 wavamia na kuziteka Bank mbili zilizo eneo moja kwa muda wa dakika 45. CRDB ambayo hata haijaanza kufanya kazi rasmi na DCB Bank
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Ilala, Ulrich Matei, ameithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba majambazi hao wanasadikiwa kuwa walikuwa kati ya 6 hadi 8.
Amesema wahalifu hao
walianza kuingia kwenye Benki ya DCB na kupora fedha zilizokuwa kaunta na muda
mchache baada ya hapo walivamia Benki ya CRDB na kupora fedha ambazo hadi sasa
haijajulikana thamani yake.
Aidha, amesema majambazi
hao waliwaua askari wawili wa Suma JKT, waliotambuliwa kwa majina ya Ramadhani
Halidi na Shane Rajabu.
"Tumeanza upelelezi
ikiwemo kuelekea katika maeneo ya Mkuranga ambapo ndiko tunakoamini kwamba hawa
wahalifu wameelekea, tutakapowakamata tutawapa taarifa kamili" Alisema
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala.
CHANZO: JAMII FORUM
CHANZO: JAMII FORUM



No comments:
Post a Comment