HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » UPDATES: TRA YATOA MASAA 24 KWA MMILIKI WA MAKONTEUNA 9 YALIYOKAMATWA KUJITOKEZA,VINGINEVYO WATAYATAIFISHA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato nchini TRA Richard Kayombo ametolea ufafanuzi juu ya kukamatwa kwa makontena 9 katika eneo la Mbezi Tank Bovu jijini Dar es Salaam ambapo mpaka sasa hivi Makontena hayo pamoja na madereva waliokuwa wanayasafirisha yako chini ya ulinzi mpaka wahusika watakapojitokeza.
Kayombo amesema kuwa makontena hayo yamenaswa usiku wa manane kwa msaada wa wasamaria wema waliotoa taarifa za kupakiwa kwa makontena hayo katika bandari kavu ya   PMM.
Bwana Kayombo amesema TRA imetoa masaa  24 kwa mmiliki wa makontena hayo kujitokeza, vinginevyo watayafungua na kuyataifisha kama sheria inavyoelekeza.
Amesema endapo mmiliki wa makonnteina hayo hatopatikana ndani ya masaa 24 basi makontaina hayo yatafunguliwa na kutazama mali zilizomo ndani ya makonteina hayo. Na kama makonteina hayo yatakuwa na bodhaa halali basi zitataifishwa na kama wakikuta bidhaa haramu basi bidhaa hizo zitateketezwa mara moja.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: