Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Duma, Areeq Amran Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mfuko mmoja wa saruji kati ya 640 aliyoitoa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule za Sekondari za wilaya hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Katika makabidhiano hayo Makonda alipokea mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Alex Malasusa aliyetoa mifuko 500.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo (kulia), akimkabidhi saruji hiyo DC Makonda.
Lori lilibeba saruji hiyo likiwa eneo la tukio.
DC Makonda na wageni wake wakiwa eneo la tukio kabla ya makabidhiano ya saruji hiyo.
Mhe. Bulembo akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo.
Wanahabari wakizungumza na watoa msaada huo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Na Dotto
Mwaibale
MWENYEKITI
wa Jumuiya ya Wazazi, Abdallah Bulembo amesema anaguswa na kazi nzuri ya
utekelezaji wa Ilani ya CCM inayofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul
Makonda katika ujenzi wa shule za sekondari za kata.
Bulembo
ambaye pia ni Mjumbe wa kamati kuu ya CCM alisema kutokana na jitihada hizo
ameona haja ya kumtia moyo Makonda kwa kuchangia ujenzi wa shule hizo saba
unaoendelea.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi saruji mifuko 500 Bulembo alimtaka
Makonda kuendelea kupigania utekelezaji wa Ilani bila kujali itikadi za vyama
katika kuleta maendeleo ya wilaya hiyo.
Alisema
Jumuiya ya wazazi kazi yake kubwa ni ulezi hivyo mafanikio yatakayopatikana
kutokana na wanafunzi zaidi ya 3183 waliokosa shule katika wilaya hiyo kuweza
kuendelea na masomo ni ya kujivunia.
Aliwataka
watendaji wa Manispaa hiyo kuhakikisha malengo ya ujenzi huo yanatimia ili
kuokoa watoto ambao wangeathirika kutokana na kukosa elimu.
Makonda
aliwapongeza wote wanaojitokeza katika kumuunga mkono katika ujenzi wa shule
hizo na kusema jana amepokea mifuko 1640 ya saruji.
Alisema
saruji hiyo ni mifuko 500 kutoka kwa Bulembo,500 kutoka kwa aliyekuwa Askofu
Mkuu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Alex
Malasusa na mifuko 640 kutoka Kampuni ya The Duma Group.
Aliwahakikishia
wadau hao wa elimu kuwa atasimamia ipasavyo ujenzi wa shule hizo ili kupunguza
wimbi la watoto wasio na elimu Kinondoni ambao ndio chimbuko la vijana
wanaotumia dawa za kulevya,biashara ya ngono,vibaka,mimba za utotoni na wahalifu
wengine.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya The Duma Group, Areeq Amran Mohamed alisema lengo la kusaidia
saruji hiyo ni kuungana na serikali katika kutekeleza sera ya kuinua elimu
wilaya ya Kinondoni.
(Imeandaliwa
na mtandao wa www. habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment