Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi
akiwasikiliza wafanyabiasha wadogowadogo waliofika kueleza matatizo yao
yanayowakabili kuhusu Halmashauri ya Mafinga.

Wafanyabiasha wadogowadogo wakiwasikiliza Mbunge
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi walipokutana naye walipokuja kutoa
malalamiko yao.
NA FREDY MGUNDA, MAFINGA
Mvutano mkali kati ya wafanyabiashara wadogowadogo (machinga) mjini Mafinga mkoani Iringa na uongozi wa halmashauri hiyo umeendelea kufukuta baada ya wafanyabiashara hao kugomea kuondoka katika
eneo hilo wakidai maslai ya watu wachache ndio yanayowahamisha katika eneo hilo
jambo lilopelekea mbunge kuingilia kati .
Wakitoa kilio chao mbele ya mbunge wa mafinga mjini Mh. Cosato Chumi
wafanyabiashara hao walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kwa muda mrefu na
halmashauri hiyo kwa kuhamishwa hamishwa kila kukicha na kupelekwa
maeneo ambayo siyo rafiki kwa biashara zao .
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Glibet Amoni alisema
hapo awali walikuwa wakifanyia biashara zao bembeni ya soko la mafinga Uwanja
wa mashuja na badaye kuja kuhamishwa katika eneo hilo na kupelekwa katika
eneo la Kinyanambo ambalo pia halifai kwa biashara kwa kuwa kipindi cha mvua
vitu vyao huzama kwenye maji kwa kuwa eneo hilo huwa linasimamisha maji pindi
mvua inyeshapo .
Alisema kuwa baada ya kuona eneo hilo linaharibu biashara zao
waliamua kurudi katika eneo lao la awali la mashuja na kuutaarifu uongozi wa
halmashauri hiyo kuwa wamerejea katika eneo hilo lakini walifanya
biashara kwa majuma mawili na baadaye kuja kutangaziwa kuondoka katika eneo
hilo na kwenda katika soko jipya ambalo pia miundombinu yake haijakamilika na
wali sio eneo la wamachinga
Alisema kuwa walishanga kusikia matangazo ya barabarani kuwa
hakutakuwa na mnada katika eneo hilo siku ya jumapili na walipokwenda siku hiyo
walikuta magari ya polisi yakiwa yametanda katika eneo hilo kuwazuiya kufanya
biashara katika eneo hili jambo lililozidi kuwadhofisha kwa kuwa wengi wao wana mikopo katika maeneo mbalimbali na wanapaswa kurejesha mikopo hiyo
“Mh mbunge wewe ndio msaada wetu uliahidi kututetea sana tunaona
kuna mambo ya siasa yanaingia hapa kwani huyu mwenyekiti wa halmashauri
Charles Makoga anatulazimisha kwenda kule kwa kuwa yeye anavibanda vyake kule
sokoni ndio mana analazimisha tupelekwe kule na tushanga kuja
kututangazia kibabe na kuondolewa na polisi kama vile ni majambazi wakati
ushuru wao tunalipa na eneo huwa tunafanya usafi kwani wanatufanyia hivii au
sisi sio watanzania ”
Waliongeza kuwa wao siku yao ya kufanya biashara ni siku moja
tu ya wiki yani jumapili lakini wameshanga kuona uongozi wa halmashauri hiyo
kwa kushirikiana na wafanyabiashara wachache wa soko kuu wanaolalamika kutokuuza
bidhaa zao pindi mnada huo unapofanyika katika eneo jambo ambalo siyo la kweli.
Akipokea kilio cha wafanyabiashara hao mbunge huyo wa Mafinga mjini Mh. Cosato Chumi
aliwataka wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu ili kuweza kwenda kuzungumza na
uongozi wa halmashauri hiyo ili kuona ni sababu gani zilizopelekea wao
kutolewa katika eneo hilo na kupelekwa soko jipya eneo ambalo limetegwa kwa
ajili ya soko na wala sio kwa ajili ya mnada wa siku moja .
Chumi alisema yeye kama mbunge hatokubali kuona wananchi wake
wananyanyaswa na watu wachache kwani yeye ni mbunge wa watu wote na wala
hatakubali kuona watu wake wakipelekwa katika maeneo ambayo siyo rafiki kwa
biashara
‘’Kilio chenu nimekisikia na mimi nataka kukimbizana na kasi ya Rais Magufuli ya kuwatetea wanyonge sioni sababu za msingi za nyie kuhamishiwa kule
soko jipya wakati nyie huwa munafanya mnada siku moja tu hao wanaosema hawauzi
kwanini wanakuwa wabinafsi hivyo wao wanauza siku sita nyie mnada wenu
ni siku moja halafu eti wanasemna hawauzi mi niwambie waache ubinafsi
na hili sitakubaliana nao ’’
Chumi alisema kuwa kimahesabu kupeleka mnada katika eneo hilo
lililojengwa kwa kwa ajili ya soko ni kupoteza mapato ya halmashauri kwani
badala ya kukusanya ushuru wa siku saba kwa wiki watakuwa wanakusanya ushuru wa
mnada ambao ni siku moja kwa wiki jambo ambalo kimahesabu halikubaliki
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Jimsoni Mhagama
alisema inapaswa busara kutumika katika kuwasimamia wafanyabiashara hao na
kuchana na kutumia ubabe kwani nao wanahaki ya kufanyabiashara kama
wanavyofanya watu wengine .
Mhagama alisema kuwa serekali ya Raisi Magufuli ni serekali
inayowangalia wafanyabiashara wadogo kwa jicho la pili ili waweze kufanikiwa
katika biashara hao na kuwanyanyasa au kuwahamisha bila ya kukaa chini na
kukubaliaba siyo jambo la busra na ofisi yake atajaribu kuangallia jinsi gani
ya kuwasaidia ili wafikie muafaka



No comments:
Post a Comment