Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi
Mkoa wa Iringa, Ephraam Mhekwa akihutubia wananchi wa Kijiji cha
Lulanzi wilayani Kilolo, mkoani Iringa wakati sherehe za uzinduzi wa
maadhimisho kimkoa ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM. (Picha
zote na Friday Simbaya)
MAADHIMISHO ya kumbukumbu ya miaka 39
ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimkoa yamezinduliwa Januari
31, mwaka huu, na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Iringa,
Ephraam Mhekwa katika Kijiji cha Lulanza wilayani Kilolo, Mkoa wa
Iringa.
Aidha, kilele cha maadhimisho hayo
kinatarajiwa kufanyika mkoani Singida, Februari 6, mwaka huu, na mgeni
rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais mstaafu Jakaya
Kikwete.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa
wa Iringa, Ephraam Mhekwa alisema mgeni rasmi katika kilele cha
maadhimisho kimkoa mgeni rasmi atakuwa mlezi wa mkoa ambaye ni waziri
mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Tanzania Mzengo Pinda.
Alisema pia kuwa kilele cha
maadhimisho hayo kimkoa yatafanyika katika Jimbo la Isimani wakati
mwaka jana yalifanyika katika Jimbo la kalenga wilayani
Iringa.
Alisema kuwa mambo yanayotakiwa
kuzingatiwa katika wiki hiyo ni pamoja na kuingiza wanachama wapya wa
CCM na jumuia zake na kufanya shughuli zingine za kuimarisha
Chama.
“Shughuli nyingine inayotakiwa katika
wiki ya maadhimisho ni kufanya mikutano ya kuwashukuru wana-CCM na
wananchi kwa kuiamini CCM na kuhamasisha wananchi kufanya kazi za
maendeleo,” alisema Mhekwa.
Aliongeza kuwa katika maadhimisho hayo
yaliyobeba kaulimbiu ya ‘sasa kazi, kujenga nchi na kukijenga Chama’
ni pamoja na kushiriki katika ujenzi wa madarasa, vituo vya afya,
zahanati, upandaji miti, uchimbaji wa mitaro ya maji na kufanya usafi
wa mazingira.
Alisema kilele cha sherehe hizo
zitafanyika Februari 6, mwaka huu, kwa kuwa Februari 5, ambayo ndiyo
siku CCM ilianzishwa, itakuwa ni siku ya kazi.
Pia, alitumia fursa hiyo kuwaomba
wana-CCM, wadau na wananchi wengine kwa ujumla, kushiriki kikamilifu
maandalizi na wahudhurie kwa wingi sherehe hizo.
Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Iringa, Ephraam Mhekwa amekabidhi jumla ya kadi 287 kwa wana chama
wapya wakiwemo UVCCM (60), kadi za wanachama (50), UWT (77) na
wazazi (100).
No comments:
Post a Comment