Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Pichani ni mwanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Hananasif, Abdallah Mkwama. Maisha yake ni ya kusikitisha. Hayafanani na utu ambao taifa letu linahubiri. Anaishi kwenye kibanda cha mabati kilichojengwa juu ya kifusi cha iliyokuwa nyumba yao ambayo ilikumbwa na bomoabomoa katika Bonde la Mto Msimbazi, jijini Dar es Salaam.
Abdallah ni mfano wa watoto wasio na hatia, watoto wasio na makosa wanaoteseka kwa sababu ya ukatili wa mamlaka za nchi. Abdallah hakuamua yeye kuzaliwa na mzazi asiye na kipato na aliyeishia kujenga bondeni tena baada ya kupewa vibali na mamlaka hiyo hiyo iliyokwenda kubomoa.
Huwenda mtoto huyu naye angependa kuzaliwa na mzazi anayeishi Masaki kwenye jumba la ghorofa lililotokana na wizi wa fedha za umma. Ama angependa kuishi Msasani kwenye jumba la maana la baba yake ambaye amesoma vizuri na kupata fedha kihalali.
Makosa ya mzazi wake na makosa ya serikali sasa yamegeuka kuwa adhabu ya mauti kwa mtoto huyu.
No comments:
Post a Comment