HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA KUMI NA SITA (16)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Siku ile nilijitahidi sana kupiga kazi ila sikuwa sawa kabisa kifikra kutokana na maneno ya shemeji. Kuna kipindi nilikuwa nazubaa mpaka nashindwa kuwahudumia wateja vizur mpaka shemeji akaanza kugomba " Wewe mzima kweli? Nafasi kama hii wangekuwa wenzako wangeshaichangamkia na ndo pakutokea,wewe form four uliyefeli huna mbele wala nyuma unalinga? Linga" aliongea kwa minajili ya kunishawishi shemeji Nilimwangalia sana shemeji mpaka machozi yakaanza kunitokaalinishangaa sana "
 Jun naomba uende nyumbani please hatuwezi kufanya kazi ukiwa katika hali kama hii" akasema shemeji Nilikusanya kilicho changu na kisha safari ya kurudi nyumbani ikaanza,niliondoka na gari kwa sababu shemeji hajui kuendesha vizur Nilipofika njian mawazo yalinizidia sana nikajikuta nikipaki ile gari pembeni ya barabara na kuanza kulia Ni kama malaika wa shetani na wale wa Mungu walikuwa wakishindaana kunigombania Kwa sababu roho mbili zilikuwa zikishindana ndani ya kichwa changu,moja ikiniambia nimuue kweli kaka na nibaki na zile mali zote na mke wake na nyingine ikigoma "
 Kumbuka huyu ndiye ndugu yako pekee katika tumbo la mama yako,ukimuua utamuumiza sana mamako,kumbuka mlivyoishi kwa upendo tangu utoto wenu na pia kumbuka yeye ndo amekuleta mjini kukusaidia,Jun mali zinatafutwa ila uhai hautafutwi achana na mawazo ya yule shetani" hiyo ni roho ya kwanza ilivyoniambia " 
Acha ushamba Jun,wewe pekee ndiye unayeweza kucheza hii katara vizur na ukashinda utabaki milionea,kumbuka shemeji yako alivyo mtam,hakuna mwanamke kama yeye na pia kumbuka kaka yako hazalishi,hizi mali zote na huyu mwanamke ni wa kwako changamka wewe" nafsi ya pili ilinambia Nilihisi ninakoelekea ni kwenye kuchanganyikiwa kwa sababu sikuwa nikijielewa pale nilipo. 

Ndipo nikakata shaur la kwenda kunywa pombe kidogo ili japo nitoe mawazo kama nilivyosikia watu wakisema ingawa sikuwa mlevi na sikuwahi kunywa pombe Wakati najiandaa kuondoka simu yangu ya mkononi iliita kucheki ilikuwa namba ya kaka kwa sababu alikuwa anatumia Airtel ambayo hata kule Dubai ilikuwa inafanya kazi " Dogo vip? Mimi nimefika salama" alisema kaka " Tumshukuru mungu kaka hata sisi tuko salama" niliongea kinyonge mpaka kaka akanishtukia " Vip dogo kuna tatizo? Mbona unaongea kinyonge hivyo?" akasema kaka " 
Hapana sema kichwa kinanigonga sana kaka nimeondoka naelekea nyumbani kupumzika" nikamwambia " Pole sana mdogo wangu" akasema " Ahsante kaka" nikajibu " Sasa dogo nafikili unajua ni kiasi gani nakupenda mdogo wangu,hapa nilipo kuna jamaangu mmoja wa huku nimeingia naye ubia wa kibiashara amekubali kunipa vyombo vya umeme nianzishe duka na mimi nimeona hili nikpe wewe kwa hiyo nikija na hivi vifaa vitaenda kwenye duka lako nataka uwe kama mimi" akasema kaka Nilifurahi kwa kweli kwa kile alichokiongea kaka " 
Ahsante sana kaka ubalikiwe" nikasema " Usijali mdogo wangu ila nataka ukumbuke always kwamba tuko wawili peke yetu tupendane sana,nakupenda sana mdogo wangu! Chao! Baadae" akasema na kukata simu Maneno yale yalikuwa kama msumari wa moto kwenye moyo wangu,nikaanza kulia upya.

ITANDELEA  IJUMAA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: