Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kuelekea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, mjini Arusha.
Rais wa Mahakama ya Afrika Mhe. Jaji Justice Sylvain Ore akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kulinda na kutetea haki za binadamu kwa kuzingatia maazimio mbalimbali ya ndani ya nchi na ya kimataifa ikiwemo haki ya kuishi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Arusha kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati anafungua
mkutano wa mazungumzo wa masuala ya demokrasia na haki za binadamu ya Mahakama
ya Afrika ya Watu na Haki za binadamu.
Amesema
Tanzania ni mfano wa kuigwa barani Afrika kwa kuzingatia na kutekeleza ipasavyo
mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kuhakikisha wananchi wake wanapata
huduma bora na za msingi ikiwemo huduma ya afya na elimu bila kubaguliwa
kutokana na ulemavu,jinsia,rangi au dini.Amesisitiza
kuwa Serikali itaendelea kutekeleza na kuzingatia matamko mbalimbali ya Dunia
yanayolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo haki
ya kuishi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kufurahishwa na hatua zinazochukuliwa na baadhi
ya nchi za Afrika katika kulinda na kutetea haki za binadamu hasa haki za
wanawake na kusema kuwa bado kuna umuhimu mkubwa kwa nchi ambazo zinazosuasua
kutekeleza mikataba hiyo kufanya hivyo ili kuhakikisha wanawake na watoto
wanapata haki sawa katika jamii.
Wajumbe wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
Wajumbe wakipewa jarida la Mahakama ya Afrika mara baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada kuhutubia Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
No comments:
Post a Comment