HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » JE WATAKA KUJUA: JINSI MAMILIONI YA SAMAKI WANAVYOWEZA KUOGELEA KATIKA VIKUNDI KWA SPIDI KUBWA BILA KUGONGANA:

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Mara nyingi tumeshuhudia makundi ya samaki wanaofanana wakiwa kwenye makundi makubwa wakisafiri pamoja baharini. Jambo la kuvutia ni kwamba samaki hao wana uwezo mkubwa wa kusafiri kwa spidi kubwa, kukata kona kali kwa pamoja na kukaa umbali unaofanana bila kugongana.
Ni rahisi kwa samaki hao kufanya hivyo kutokana na mistari ya hisia (literal line) iliyopo ubavuni mwao, mistari hiyo inawapa taarifa kuhusu umbali na mwelekeo wa samaki mwenzake aliyepo jirani. Mistari hiyo iliyopo ubavuni hufanya kazi kama "sensor"
Pia samaki wengi wana macho pembeni mwa vichwa vyao tofauti na wanyama wengine ambao macho yapo usoni. Kitendo cha kuwa na macho upande wa kulia na kushoto kinawawezesha samaki kuona vizuri kilichopo pande zote mbili pamoja na kujua umbali aliopo jirani yake.
Macho pamoja na mistari ya hisia huwawezesha samaki wanaoogelea kwa vikundi kuweza: 



1.Kusafiri sambamba na wengine. Wanasonga kwa mwendo sawa na samaki walio kando yao na kudumisha umbali unaofaa kutoka kwao.



2.Kuepuka kugongana. Wanabadili upande wanaoelekea ili kuepuka kugusana na samaki wengine.


3. Kuepuka kuliwa na samaki wakubwa, samaki mwenye umbo dogo anapotembea peke yake anajiweka katika hatari ya kuliwa na samaki wakubwa, hatari ya kuliwa huwa ndogo wanaposafiri katika makundi na katika spidi kubwa.


Kwa kutegemea tabia hizo tatu za samaki wanaoogelea katika vikundi, watengenezaji wa magari nchini Japani wamebuni magari kadhaa madogo ya roboti yanayoweza kusonga katika kikundi bila kugongana. Badala ya macho, roboti hizo zinatumia teknolojia ya mawasiliano; badala ya mstari wa chembe za hisi, zinatumia leza inayotambua umbali. Kampuni hiyo inasadiki kwamba teknolojia hiyo itawasaidia kutokeza magari “yasiyoweza kugongana” na “kusaidia mazingira yasiharibiwe na pia kusiwe na msongamano wa magari.”

Imeandaliwa na Moses Mutente

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: