HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » SUMU YA PENZI SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA(41)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Alianza kuja Catherine, nikaanza kumbana anielekeze nini kilichotokea juzi usiku huku nikiwa makini kutomtaja moja kwa moja mume wangu wala Fatuma.
“Mh kwani Mary una maanisha nini? kwa sababu siku ile kulikuwa na vituko vingi sana,” alisema Catherine.
“kama vituko vipi?”
“Mh kama mumeo kuanza kuongea kingereza baada ya kulewa, kingine wewe kulewa savannah nne na kulala,” alisema Catherine lakini sikutaka hayo, nilitaka aniambie kuhusu Fatuma, basi nikatengeneza swali ili mradi tu asinishtukie maana yangu kuwa eti ninahisi naibiwa mume na Fatuma maana itakuwa aibu.
“Niambie kuhusu Fatuma, alikuwaje siku ile.” Niliuliza tena.
“mh sijui kama nitakumbuka vizuri maana mimi mwenyewe nilikuwa nimelewa kweli, lakini Fatuma alikuwa mtambo noma! alikunywa ile mbaya na ilivyokuwa chukuchuku yule lazima aliondoka na mtu pale baa.”
“Chukuchuku ndiyo nini? aliondoka na nani?” nilijikuta nauliza harakaharaka huku mapigo ya moyo wangu yakinidunda kwa kasi.
“shoga na wewe, huo umarekani umekukosesha mengi! Chukuchuku maana yake ni msichana rahisirahisi kuwavulia nguo wanaume,” alisema Catherine moyo ukanifanya “Pah!”




UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMAPILI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: