Mamba wanakula mawe ili kusaidia mchakato wa kusaga chakula tumboni. Mara nyingi mamba hupenda kumeza vitu vikiwa vizima vizima, hawana muda mwingi wa kutafuna nyama. Ili chakula hicho kiweze kusagika vizuri tumboni mamba hulazimika kumeza mawe ili yasaidiane na nyongo iliyopo tumboni ili kusaga chakula hicho.
Mawe hayo hukaa miaka mingi sana tumboni mwa mamba, na wakati mwingine mawe hayo humwongezea uzito na kumsaidia mamba kuzama vizuri kwenye maji yenye kina kirefu. Wakati wa upungufu wa chakula mamba hutumia mawe yaliyopo tumboni mwake kama njia ya kumuepusha na ukali wa nyongo inayomwagika kwa lengo la kusaga chakula, kitendo hicho hufanya mawe hayo yawe 'smooth' sana pindi yanapotolewa tumboni mwa mamba. Kitaalam mawe hayo huitwa 'Gastrolith'
IMEANDALIWA NA MOSES MUTENTE
No comments:
Post a Comment