Mwanahisa wa Jamii Media Co Ltd, Mickey William ameunganishwa katika kesi mbili zilizokuwa zinamkabili mkurugenzi mtendaji wa mtandao huo, Maxence Mubyazi za kuzuia uchunguzi wa jeshi la polisi.
Wakili wa Serikali, Mohammed Salum alidai kuwa washtakiwa hao wakiwa katika eneo la Mikocheni kwa nafasi zao na wakijua jeshi la polisi linafanya uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao ambayo yalichapishwa katika tovuti yao kwa njia ya kuzuia uchunguzi huo walishindwa kutekeleza amri ya kutoa data walizonazo.
Upelelezi wa kesi hizo umekamilika washtakiwa watasomewa maelezo ya awali Februari 9 na 20, 2017. Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana
No comments:
Post a Comment