HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » SUMU YA PENZI SEHEMU YA AROBAINI NA TANO(45)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Wakati najiuliza maswali hayo nikamuona Hadija akiwa yupo mbali kweli kimawazo, ikabidi nimshtue kwanza.
“we Hadija vipi?” nilimgusa akaonekana kurudisha akili yake kwenye maongezi yetu.
“Yaani shoga ndo nakumbuka aisee, sikutarajia!” alisema Hadija nikatulia bila kumuuliza mwenyewe akafafanua: “sikia, Fatuma na mimi kama nilivyokwambia hapo mwanzoni, tulichezwa unyago pamoja, na hayo mengi aliyomfanyia Steve naona aliyatoa kule unyagoni. Nilikuwa najuaga ni utani kumbe ni ya ukweli, Mh!” “we Hadija kwa hiyo kweli kuna mtu anaweza kufundisha hayo mambo mtu akawa kama Fatuma?” niliuliza kwa shauku.
“Ndiyo wanafundisha, mimi na Fatuma tulifundishwa tukiwa wadogo hivi nakumbuka mimi nilikuwa na miaka 7 na Fatuma alikuwa na miaka 14 , tukiwa wote Masasi,” alinijibu, Steve akawa anashangaashangaa tu akili yake ikiwa ipo kwa Fatuma tu, ikabidi tumruhusu aondoke wakati huo mimi na Hadija tukaanza kuongea mambo ya kujenga.
“Sasa Hadija mimi nilikuwa nataka sana kufundishwa na huyo Kungwi kama yupo popote nipo tayari kwenda,” nilimwambia Hadija akashangaa kuona nipo siriazi ile mbaya.
“Mh, sidhani kama kwa mtu mzima kama wewe atakubali, lakini mimi ninachojua kwetu Wamakonde wanafundisha kuanzia umri wa miaka 7 hadi 15 siyo kwa mtu aliyeolewa kama wewe.” Alisema Hadija.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA


ITAENDELEA ALHAMISI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: